SUDAN na SUDAN KUSINI zakubaliana kufungua mpaka:;
Sudan na Sudan Kusini zimekubaliana kufungua mpaka kati ya nchi hizo mbili na kuongeza muda wa mkataba wa kusafirisha mafuta
Sudan na Sudan Kusini zimekubaliana kufungua mpaka kati ya nchi hizo
mbili na kuongeza muda wa mkataba wa kusafirisha mafuta ambao
utaiwezesha SUDAN Kusini kutumia mabomba ya SUDAN kusafirisha mafuta.
Makubaliano hayo yamefikiwa wakati wa ziara ya makamu wa Rais wa
SUDAN Kusini TABAN DENG GAI nchini SUDAN ambapo alifanya mazungumzo na
Rais OMAR AL-BASHIR kuhusu usalama, ushirikiano kati ya nchi hizo na
makubaliano ya masuala ya mafuta.
Waziri wa Ulinzi wa SUDAN, KUOL MANYANG JUK amesema nchi hizo
zimekubaliana kufungua mkapa huo katika kipindi kisichozidi siku 21 na
kwamba SUDAN Kusini imehakikisha kuwa waasi wa nvhini humo hawataingia
SUDAN
Uhusiano kati ya nchi hizo mbili ulizorota na kusababisha
mpaka kufungwa tangu SUDAN KUSINI ilipojitenga kutoka SUDAN Julai
2011.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!