UONGOZI wa klabu ya Simba umemwandikia barua mfanyabiashara Mohamed
Dewji, ‘Mo’ kutaka kujadiliana naye juu ya nia yake ya kununua hisa
asilimia 51 za klabu hiyo kwa Sh bilioni 20.
Katika barua yake hiyo iliyoandikwa na Katibu Mkuu wa Simba, Patrick
Kahemele ilimtaka Mo kuwasili Agosti 15 katika Hoteli ya Serena kwa
ajili ya majadiliano hayo na Kamati ya Utendaji.
Mo ambaye aliwahi kumiliki timu za African Lyon pamoja na Singida
United, ameonesha nia ya kununua hisa hizo jambo linaloonekana kuwavutia
wanachama wengi wa klabu hiyo.
Juzi katika Mkutano Mkuu wa wanachama uliofanyika Bwalo la Maofisa wa
Polisi Oysterbay, hoja kubwa ilioonekana kuutawala mkutano huo ni
uuzwaji wa hisa hizo ambapo ilisababishaa wanachama kuvuruga kujadiliwa
kwa hoja nyingine.
Wanachama wengine wakiwa wamevalia fulana zisemazo ‘Mpeni Mo timu
yake’ huku wengine wakipiga kelele wakilitaja jina la Mo, walizua
tafrani hali iliyosababisha rais wa klabu hiyo, Evans Aveva kuahirisha
ujadiliwaji wa hoja nyingine na kusisitiza kuwa hoja ya mabadiliko
imekubaliwa na kuwa timu hiyo inaanza mchakato wa uendeshwaji katika
mfumo wake mpya.
Baada ya hoja hiyo, jana asubuhi Mo alifanya mkutano na waandishi wa
habari ofisini kwake akiweka wazi kuwa ameshaandika barua rasmi ya
kutaka kununua hisa hizo huku akiwapa miezi mitatu Simba kumpatia jibu.
Mo alisema amekuwa na nia ya kununua hisa muda mrefu kwa kuwa akiwa
kama mwanachama wa klabu hiyo anaona kuwa kuna udhaifu mkubwa kwa sasa
ambao unatakiwa kukabiliwa.
Saa chache baada ya mfanyabiashara huyo ambaye ni kati ya
wafanyabiashara vijana wakubwa barani Afrika kumaliza mkutano wake huo,
Simba ilituma barua kwa vyombo vya habari inayoelezea kumuita kikaoni
Mo.
Barua hiyo ilisema kuwa imeamua kumwita kikaoni Agosti 15 kwa kuwa
wiki ya kwanza ya mwezi huu klabu hiyo itakuwa na shughuli nyingi za
kufanya na hasa maandalizi ya Simba day inayotarajiwa kufanyika Agosti
8. Pia ilifafanua kuwa kwa sasa inashughulikia usajili na hivyo kuongeza
kuwa ina imani kuwa tajiri huyo atafika kwa kikao Agosti 15.
Mo katika kikao chake za asubuhi alisema kuwa kwa sasa anachotaka ni
kuona maendeleo ya Simba na sio vinginevyo na kuongeza kuwa akipewa
nafasi atahakikisha anawekeza fedha, muda na mapenzi yake yote kwa klabu
hiyo.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!