PROGRAMU YA SIMU YA UZAZI WA MPANGO,NJIA YA ASILI:;
Matumizi ya kupanga uzazi kwa njia ya
kalenda yaweza kuwa na ugumu kufuatilia wakati mwingine kutokana na
majukumu mbali mbali ya kimaisha. Programu za simu (mobile apps) zaweza kutumika na kukurahisishia na kuweza kutumia njia ya kalenda kwa usahihi.
CycleBeads® ni programu ya simu zinazotumia mfumo wa
Android na
hutumika kusaidia wanafamilia kupanga uzazi. Programu hii imebuniwa na
idara ya afya ya uzazi katika chuo kikuu cha Georgetown na imetengenezwa
maalum ambayo ni rahisi kutumia na ya uhakika kwa kina mama kupanga na
kuzuia ujauzito kwa kutumia njia ya
asili.
Utafiti uliofanyika umeonyesha kuwa njia hii imeweza kuwa na usahihi wa
zaidi ya asilimia zaidi ya 95 hii ikiwa ni sawa au zaidi ya njia
nyinginezo zitumikazo kuzuia ujauzito.

Sharti la kitabibu la kutumia programu hii ya simu za
android
ni kuwa mwanamama awe na mzunguko wa hedhi wa kati ya siku 26 hadi 32 .
Inakadiriwa kuwa 80% ya kinamama wote huwa kati ya siku hizo
zilizotajwa. Endapo mwanamama atakuwa na mzunguko wa hedhi katika mwaka
ambao ni pungufu ya siku 26 au zaidi ya siku 32, programu hii haitakuwa
na ufanisi. Kama hauna uhakika na mzunguko wa hedhi inabidi uanze
kufuatilia kwa kuweka rekodi kabla ya kuanza kutumia programu hii. Kama
umejifungua karibuni au ulikuwa unatumia njia za homoni za uzazi wa
mpango inabidi usubiri hadi pale mzunguko wa hedhi utakapokuwa umerudi
kawaida(kati ya siku 26 hadi 32 za mzunguko wa hedhi),kabla ya kutumia
programu hii.
Baada ya kupakua na kusimika programu hii katika simu yako, mwanamama
huitajika kuingiza tarehe ambayo alianza kuona siku zake za hedhi, na
programu hii humuonyesha siku zilizo salama na zile ambazo mwanamama
anaweza kupata mimba.
Waweza kupakua programu ya CB kutoka
google play store au tembelea mtandao wa
www.cyclebeads.com kwa maelezo zaidi.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!