Ofisi za Bunge kuhamia Dodoma Septemba mwaka huu:;
Ofisi za Bunge zilizopo Jijini Dar es salaam zinatarajia kuhamishiwa
Dodoma mwezi Septemba mwaka huu, ikiwa ni utekelezaji wa agiza la Rais
Magufuli la kuhamishia shughuli za serikali Dodoma.
Taarifa hiyo imetolewa na Spika wa Bunge, Job Ndugai jana na kusema
kuwa kwa bunge suala la luhamia Dodoma siyo gumu kwa kuwa tayari makao
makuu yake yako Dodoma.
Alisema tayari alikwishatoa maagizo kwa ofisi yake kuhakikisha kuwa
kufikia mwezi Septemba kila kitu kinachofanyika Dar es salaam kifanyike
Dodoma isipokuwa mambo machache.
“Nimeagiza ofisi yangu ihamie dodoma mara moja kuanzia Septemba hii,
watumishi wa bunge karibu wote watahamia Dodoma, masuala ya malipo
yataangaliwa baadaye, kwa sasa ni kuhamia dodoma tu, ofisi tunazo huko”
Alisema Ndugai
Kama sehemu ya mwanzo wa utekelezaji wa azma hiyo, tayari ofisi ya
bunge imetangaza kufanyia Dodoma vikao vyake vyote vya kamati za bunge
tofauti na ilivyokuwa umepangwa mwanzo na ilivyozoeleka kufanyikia Dar
es salaam.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!