
Ubuyu wa mjini unanyetisha kuwa, mkali wa Bongo Fleva anayetamba na
wimbo wake wa Jike Shupa aliomshirikisha Ali Kiba, Natfal Mlawa ‘Nuh
Mziwanda’, anadaiwa kupora demu wa jamaa ambaye naye ni msanii wa wa
Bongo Fleva, Valentino Michael ‘Vale wel’.
Mrembo anayedaiwa kuporwa kwa Vale ni yule Nawali ambaye kwa sasa Nuh anamnadi kuwa ni mpenzi wake wa kiyama.
Ubuyu ulionaswa na Wikienda ulidadavua kuwa mwenye demu wake alipigwa na
butwaa alipomuona Nuh akimnadi Nawali kwenye mitandao ya kijamii ndipo
akang’atwa sikio kuwa kwa sasa hana chake kwani ‘mtoto’ yupo mikononi
mwa Nuh.
Akimwaga chozi mbele ya Wikienda, Vale alisema kuwa mpaka sasa hajaelewa
ni kwa nini Nuh ameamua kumtangaza Nawali kuwa ni mpenzi wake wakati
akijua wazi kwamba ni shemeji yake na ni mwanamke wake wa siku nyingi
kwani wanafahamiana.
“Kiukweli nilikuwa sijui hili wala lile. Nilipoingia mitandaoni
nilipigwa na butwaa kumuona Nuh akijitangazia ufalme kuwa mpenzi wake
kwa sasa ni Nawali.
“Mwanzoni nilijua labda ni mambo ya kiki kwa sababu nijuavyo Nuh hana malengo mazuri na Nawali.
“Baadaye ndipo nikawa nahakikishiwa na watu wangu wa karibu kuwa ni wapenzi na hawafanyi kificho.
“Kinachoniumiza nilikuwa sina tatizo wala ugomvi wowote na Nawali na
bado naamini ni mpenzi wangu kwa sababu hatujaachana na tukikutana huwa
tuko kama kawaida,” alisema Vale.
MWENYE KISU KIKALI?
Vale alizidi kutokwa povu kuwa kwa sasa hasemi sana kwa sababu hana
mkwanja wa kumpa Nawali hivyo ule usemi wa mwenye kisu kikali unamtafuna
kwani inawezekana Nuh anatumia vijisenti alivyonavyo kumnyang’anya
tonge mdomoni.
“Lakini ukweli ni kwamba ‘nafaiti’ na mambo yatakaponinyookea
nitahakikisha nafanya kila njia kumrudisha Nawali kwenye himaya yangu
kwani ndiye mwanamke wa maisha yangu.
“Najua nilipomtoa, ni mwanamke ambaye ninampenda sana na nimetumia muda
mwingi kumbadilisha kimuonekano kwani mwanzoni hakuwa alivyo sasa,
alikuwa mgumu hivyo nimefanya jitihada za hali ya juu kumfanya aonekane
‘soft’,” alimalizia Vale.
Mwanaume anayedai kuibiwa akiwa na niwale enzi zao HUYU HAPA MTUHUMIWA NUH
Baada ya ubuyu huo ulionyooka kutua kwenye Wikienda, waandishi wetu
walimweka ‘mtukati’ Nuh aliyedai kuwa hapendi kumuongelea mpenzi wake
huyo kwa sababu kama ni maneno yameshasemwa mengi.
“Unajua kuhusu huyu demu wangu, maneno mengi sana yamesemwa hadi
nimechoka. Kama huyo mwanaume yupo na anaamini ni mwanamke wake basi
amchukue akakae naye,” alisema Nuh akiomba kuachwa atulize mawazo.
NAWALI ANASEMAJE?
Kwa upande wake Nawali, alipotafutwa kwa njia ya simu alisema kuwa
hamjui Vale na wala hajawahi kupiga naye picha za kimahaba ambazo gazeti
hili lina nakala zake.
Habari kutoka kwa Wana-Ubuyu wanaolinyaka vilivyo sakata hilo wanadai
kwamba Vale ana uhakika kuwa huyo ni mpenzi wake na picha ametoa wakiwa
wawili tena kimahaba hivyo inakuwaje Nawali anabisha?
HUYU NDIYE NUH
Mbali na Nawali, baada ya kufungishiwa virago na Zuwena Mohammed
‘Shilole’, Nuh alitua kwa mrembo mwingine shombeshombe ambaye hata hivyo
hawakudumu
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!