MATABIBU wanne wa Tiba Asilia na Mbadala akiwemo mmiliki wa Kliniki
ya Sure Herbal, Simon Rusigwa wamewasilisha maombi ya kuomba ruhusa ya
kufungua kesi ya kupinga uamuzi wa kufutiwa leseni za kutoa huduma za
kitabibu.
Wamewasilisha maombi hayo katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya
Dar es Salaam, dhidi ya Baraza la Tiba Asilia na Mbadala, Katibu Mkuu wa
Wizara ya Afya na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).
Mbali na Rusigwa, matabibu wengine waliowasilisha maombi hayo kupitia
kwa Wakili Dk Lucas Kamanija, ni Abdallah Mandai wa kliniki ya Mandai
Herbalist, Fadhili Kabujanja wa Fadhaget Sanitarium na John Lupimo wa
Lupimo Sanitarium.
Maombi hayo yalitakiwa kusikilizwa jana mbele ya Jaji Ama–Isario
Munisi wa mahakama hiyo, hata hivyo kabla ya kuanza kusikilizwa,
Serikali iliwasilisha pingamizi la awali ikidai kuwa maombi hayo
hayakufuata misingi ya kisheria.
Katika pingamizi hilo serikali inadai kuwa maombi hayo yana kasoro
kwa kuwa waombaji hawajapita njia zote zinazotakiwa wazifuate ndipo
waende mahakamani pia wanadai maombi hayana miguu ya kusimamia kwa kuwa
hati ya viapo vya walalamikaji vina upungufu ya kisheria.
Baada ya kuwasilishwa kwa pingamizi, Jaji Munisi aliahirisha shauri
hilo hadi kesho saa 8 mchana, ambapo alizitaka pande zote zinazohusika
ziwepo ili kusikiliza pingamizi hilo.
Katika maombi yao, matatibu hao wanadai, wameamua kupeleka maombi
hayo mahakamani, kwa kuwa wanaamini walifutiwa leseni bila kufuata
taratibu za kisheria.
Wamedai wanaamini uamuzi uliochukuliwa umetolewa bila kupitia Kamati
ya Maadili ya Baraza la Tiba Asilia na Mbadala, huku wakidai kuwa huo si
uamuzi bali zilikuwa tuhuma mpya, lakini hawakupewa nafasi ya
kusikilizwa.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!