WANACHAMA wa Yanga jana wameweka historia ya aina yake baada ya
kuridhia kumkodishia klabu hiyo kwa miaka 10 mwenyekiti wao, Yusuf
Manji. Uamuzi huo umefikiwa katika Mkutano Mkuu wa dharura uliofanyika
jana kumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.
Manji ameomba apewe klabu kwa miaka 10 na katika kipindi hicho
atakuwa anachukua asilimia 75 ya mapato ya timu, huku asilimia 25
ikibaki kwa wanachama. Na katika kipindi hicho cha miaka 10, timu ya
soka na nembo ya klabu zote zitakuwa chini ya kampuni zake.
“Mkinikodisha ndani ya miaka mitatu nitahakikisha naingiza faida, na
asilimia 25 ya faida itakwenda kwenye klabu, ikiwa ni hasara nitabeba
mimi, na baada ya miaka 10 nitawarudishia klabu yenu muanze kununua
hisa,”alisema Manji.
Aidha, Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la klabu hiyo, Francis Kifukwe
alisema baada ya wanachama kuridhia mpango huo wao wanampa pia ridhaa
hiyo Manji.
Yanga yadaiwa bilioni 5.445/- Awali kabla ya kuomba ridhaa ya
wanachama wa klabu hiyo kumkodisha timu Manji, alisoma taarifa ya fedha
ambazo zimetokana na wadhamini wao Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) ambazo
ni Sh milioni 500, Vodacom Sh milioni 73, mauzo ya wachezaji Sh milioni
74 na mapato ya mlangoni Sh milioni 678 zinazofanya jumla ya makusanyo
yote kufikia Sh bilioni 1.325 wakati matumizi ambayo ni mishahara ya
wachezaji, usajili, posho na gharama za usafiri ambazo jumla ni Sh
bilioni 2.879.
“Yanga imekuwa na upungufu wa Sh bilioni 1.5 na klabu imekuwa ikikopa
bila riba na imekuwa ikikopa kwa miaka 10 iliyopita na imeshindwa
kulipa.
“Kwa mwezi Agosti klabu inahitaji Sh milioni 500 ya kuendesha
shughuli mbali mbali za klabu ukiacha Sh milioni 88 za udhamini wa
Quality Group ambayo inaweka nembo yake kifuani kwenye jezi ya Yanga.
“Klabu imekuwa ikijiendesha kwa hasara kila mwaka, hizi fedha zinazodaiwa watauza majengo ili wazilipe?” alihoji.
“Yanga hainunuliki, Yanga si ya mtu mmoja ni ya watu wote, naombeni
ridhaa yenu niikodishe kwa miaka 10 iwe chini ya kampuni zangu,
nitachukua asilimia 75 ya faida na klabu nitawapa asilimia 25,”alisema
Manji akishangiliwa na wanachama waliofurika ukumbini hapo.
Afukuza wajumbe
Katika mkutano huo pia Manji aliwaambia wanachama wa klabu hiyo ya
mtaa wa Twiga na Jangwani kuwa hawezi kufanya kazi na wajumbe mizigo na
wanafiki na kutaka wanachama wampe ridhaa ya kuwafukuza na kuwavua
uwanachama wajumbe watatu, kitu ambacho alikubaliwa.
Wajumbe waliotimuliwa ni Ayoub Nyenzi ambaye pia ni mjumbe wa kamati
ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Salum Mkemi na Hashim
Abdallah. Baada ya kutamka hivyo, Hashimu ambaye alikuwa amekaa meza kuu
alinyanyuka na kuondoka huku akijikuta akipata adha kubwa ya kuzomewa
na wanachama hao wa Yanga.
Aishukia TFF
“Baada ya mchezo wa Kombe la Shirikisho kati ya Yanga na TP Mazembe,
TFF ilisema itachukua jukumu la kusimamia maandalizi ya michezo yetu ya
kimataifa, mechi yetu ya Medeama maandalizi jumla ni Sh milioni 170
tumewapelekea TFF na mpaka leo hawajatulipa gharama zetu kama
ilivyoahidi.
“Tangu mwaka 2013 tumejiandikisha kwenye mfumo wa VAT tumekuwa
tukiingia gharama zote za kodi na hatujawahi kupokea kodi zetu kutoka
kwenye mapato ya mlangoni…
“Mapato ya mlangoni lazima tuyaingize kwenye vitabu vyetu vya fedha
na benki kama mapato, tunayoainisha na kodi zinatokana na manunuzi na
hivyo kupaswa kuyapokea na kuyawasilisha TRA kwa kufunguliwa jalada,
jumla ya VAT kwenye mapato ya mlangoni tunapaswa kupewa na TFF ni Sh
milioni 382 ambazo hawajatupa.
Amkingia kifua Muro
“TFF wamemfungia Muro, wamekuwa wakiitendea Yanga mambo mabaya, mpaka
leo hakuna nakala ya hukumu iliyowasilishwa, sasa nasema hivi, Muro
ataendelea kufanya kazi Yanga, mimi ndio nimemuajiri, kama ni kumfungia
basi TFF wanifungie mimi,” alisema.
TFF imemfungia Muro mwaka mmoja kwa madai ya kutoa lugha za uchochezi, chuki na uchonganishi dhidi ya shirikisho hilo.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!