Sadio Mane alifunga mabao 11 alipokuwa Southampton msimu uliopita
Sadio Mane aliifungia Liverpool
bao lake la kwanza walipowabana vigogo wa Uhispania Barcelona 4-0 katika
mechi ya kirafiki huko Wembley.
Mane hakuogopa kuwepo kwa
wachezaji nyota wa Barcelona Luis Suarez na Lionel Messi katika mechi
hiyo ya kuwania kombe la kimataifa la mabingwa yaani International
Champions Cup iliyochezwa katika uwanja wa Wembley.
Mane,
aliyenunuliwa katika dirisha la uhamisho kwa kitita cha pauni milioni
£34 alifungua kivuno hicho cha mabao kunako dakika ya 15 muda mchache tu
kabla ya Javier Mascherano kujifunga mwenyewe.
Mkenya aliyebadili uraia na kuhamia Ubelgiji Divock Origi na Marko Grujic walifunga bao moja kila mmoja.
Mshambulizi wa Uingereza Daniel Sturridge hakushiriki katika mechi hiyo kwa sababu alikuwa anauguza jeraha la paja.
Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp alisema kuwa Milner alilazimika kuondoka uwanjani baada ya kujeruhiwa kisigino.
The Reds watafungua kampeini yao ya msimu mpya dhidi ya Arsenal mnamo Agosti tarehe 14 .
Hata hivyo mechi hiyo ya kirafiki iliweka historia kwa kuwa na idadi kubwa ya mashabiki.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!