Mahakama ya juu nchini Kenya imehalalisha ngono baina ya mabinamu kwa sababu inakubalika katika baadhi ya jamii nchini humo.
Mahakama
hiyo imemuachilia huru mtu mmoja aliyekuwa amefungwa kwa kosa la
kushiriki ngono na binamu yake mwaka wa 2014 kwa sababu sio makosa
nchini Kenya.
Jaji wa mahakama ya juu James Makau, alisema katika uamuzi kuwa kujamiana kwa maharimu sio haramu nchini Kenya.
''Ibara
maalum inachoshughulikia ngono ya maharimu hajata binamu kuwa mmoja wa
wale ambao kujamiana nao ni haramu maksudi, kwa sababu baadhi ya jamii
nchini Kenya zinaruhusu sio tu ngono bali hata ndo baina yao''
''jamii ya wahindi, waislamu na baadhi ya makabila humuhumu Kenya hukubali ndoa baina ya mabinamu'' alisema jaji Makau.
Bwana huyo ambaye anatambulika kama WOO alikamatwa mwaka wa 2014 kwa
kushiriki ngono na mpenzi wake wa kike ambaye pia ni binamu yake na
akahukumiwa kifungo cha miaka 10 gerezani.
''Kwa ufupi hakuna
ushahidi wowote uliotolewa kuthibitisha kuwa ngono baina ya wawili hao
ni kinyume cha sheria na kwa sababu hiyo ninaamuru mtu huyo aachiwe huru
mara moja'' hukumu ya jaji Makau.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!