
CHADEMA inapenda kutoa taarifa kwa umma kuhusu andiko linalosambazwa
mitandaoni likimnukuu Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe kuwa
ameahirisha Operesheni UKUTA na maandalizi ya Septemba 1.
Tunaomba umma upate taarifa sahihi kuwa Mwenyekiti Mbowe hajafanya
mkutano na waandishi wa habari mahali popote pale kuzungumzia kuahirisha
Operesheni UKUTA inayoendela nchi nzima wala kuzuia maandalizi ya
Septemba 1.
Kupitia taarifa hii, chama kinawataka viongozi, wanachama, wafuasi,
wapenzi na mashabiki wa CHADEMA na Watanzania wote wazalendo na wapenda
haki, kupuuza andiko linalosambazwa mitandaoni .
Msisitizo unaendelea kutolewa kuwa Operesheni UKUTA ambayo imelenga
kusimamia utawala unaoheshimu Katiba ya Nchi na kulinda sheria na
maandalizi yanaendelea nchi nzima.
Imetolewa na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA
COMMENT AND SHARE......................................................
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!