Aina tano (5) za Mazoezi Bora ya kuondoa Kitambi:;
Watu wengi wanaotaka kupunguza uzito huamini Kalori ndio kila kitu
kinachohusika. Unapochoma Kalori zaidi ya unavyokula, unapunguza uzito.
Na kama unakula Kalori nyingi kuzidi mwili wako unavyoweza kuchoma na
kutumia, mwili huongeza mafuta.
Kinachochoma Kalori mfululizo ni (Lean Muscle Mass) iliyochini ya
mafuta ya mwili ambayo huruhusu uchukuaji zaidi wa Kalori bila kuongeza
uzito.
Mwili hukubaliana na mabadiriko. Kupunguza uzito bila kufanya mazoezi
huongeza hatari ya kupoteza (Lean Muscle Mass), kupungua kwa utendaji wa
kimetaboliki na kuweka mwili kwenye hali ya kutunza mafuta.
MAZOEZI MATANO BORA YA KUONDOA KITAMBI:-
1. THE BICYCLE EXERCISE
Lala chali huku mikono yako ikiwa chini ya kichwa chako, leta magoti
yako kifuani huku ukinyanyua mabega juu. Taratibu leta kiwiko chako cha
kulia hadi kwenye goti la kushoto huku ukinyoosha mguu wako wa kulia.
Badili na upande mwingine na ufanye kama unakanyaga pedeli za baiskeli.
Fanya zoezi hili seti 1-3 kwa kurudia mara 12-16.
2. THE CAPTAIN'S CHAIR LEG RAISE
Zoezi hili huhitaji (Captain's Chair, A Rack with Padded Arms)
inayoruhusu miguu kuning'inia mara nyingi hupatikana kwenye vyumba vya
mazoezi. Kufanya zoezi hili, simama juu ya kiti (And Grip Hand Holds
Pass Back Against The Pad Then Raise Knees To The Chest To Contract The
Abs Then Lower Them Back Down.) Fanya zoezi hili seti 1-3 kwa kurudia
mara 12-16.
3. EXERCISE BALL CRUNCH
Katika zoezi hili mpira wa mazoezi ni lazima uwepo. Kufanya zoezi hili
lala juu ya mpira huku sehemu ya chini ya mgongo ikiwa imeegama vizuri.
Weka viganja vya mikono nyuma ya kichwa. Fanya zoezi hili seti 1-3 kwa
kurudia mara 12-16.
4. VERTICAL LEG CRUNCH
Kufanya zoezi hili, lala kwenye sakafu nyoosha miguu, halafu kunja
magoti, weka viganja vya mikono chini ya kichwa. Fanya zoezi hili seti
1-3 kwa kurudia mara 12-16.
5. LONG ARM CRUNCH
Kufanya zoezi hili, lala kwenye sakafu au mkeka halafu nyoosha mikono
yako nyuma iwe karibu na masikio yako. Fanya zoezi hili seti 1-3 kwa
kurudia mara 12-16.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Dah, aksante aise
ReplyDelete