YANGA jana ilizidi kujiweka pagumu kwenye michuano ya Kombe la
Shirikisho Afrika baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa
Medeama ya Ghana.
Hiyo ni mechi ya nne kwa Yanga inacheza bila kupata ushindi huku timu
nyingine kwenye kundi hilo zikishinda baadhi ya mechi zake.
Yanga ilipoteza kwa bao 1-0 katika mechi mbili dhidi ya Mo Bejaia ya
Algeria na TP Mazembe ya Congo DR kisha ikatoka sare ya bao 1-1 na
Medeama katika mechi ya kwanza nyumbani na jana ikapoteza mechi ya
marudiano na timu hiyo.
Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye uwanja wa Sekondi Takoradi,
Yanga ilionekana kuzidiwa tangu mwanzo wa kipindi cha kwanza huku beki
wake namba nne na tano wakionekana kupoteana. Medeama ilipata bao lake
la kwanza mapema katika dakika ya saba likifungwa na Daniel Amoah baada
ya kuunganisha mpira wa kona.
Wenyeji hao walipata penalti katika dakika ya tisa lakini kipa wa
Yanga, Deogratius Munish ‘Dida’ alipangua mkwaju huo. Mwamuzi alitoa
penalti hiyo baada ya nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’
kumfanyia madhambi mchezaji wa Medeama.
Dakika ya 23, Medeama ilipata bao la pili likifungwa na Abbas
Mohammed na dakika mbili baadaye Simon Msuva aliifungia Yanga bao lake
la kwanza kwa mkwaju wa penalti.
Medeama aliyoonekana kucheza kwa kasi mchezo huo kwa karibu dakika
zote za kipindi cha kwanza, waliandika bao la tatu katika dakika ya 37
kupitia kwa mfungaji wa bao la pili, Mohammed. Kipindi cha pili hakikuwa
na kasi sana na Yanga walionekana kubadilika kiasi licha ya wenyeji wao
kuwapa mashambulizi ya kushtukiza.
Kwa matokeo hayo, Yanga imeendelea kushika mkia kwenye kundi A ikiwa
na pointi moja, huku Medeama ikifikisha pointi tano sawa na Mo Bejaia ya
Algeria, inayocheza na vinara wa kundi hilo TP Mazembe ya Congo DR
wenye pointi saba leo.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!