Bondia namba moja nchini Hassan Mwakinyo, Jumamosi hii Septemba 03, 2022 atapanda ulingoni kuzichapa na bondia Liam Smith wa Uingereza katika ukumbi M&S Bank Arena ndani ya jiji la Liverpool nchini Uingereza kwenye pambano la raundi 12.
Fahamu, Mwakinyo atapanda ulingoni akizidiwa ubora, rekodi na uzoefu na mpinzani wake ila kama atashinda, Hassan Mwakinyo ataandika historia mpya kwenye ndondi duniani.
Kwa mujibu wa mtandao wa ngumi za kulipwa wa dunia (Boxrec), Liam Smith amepigana mapambano 35 na kushinda 31, amepigwa mara tatu na kutoka sare mara moja tangu 2008. Mwakinyo yeye amepigana mapambano 22, ameshinda mara 20 na kupigwa mara mbili tangu 2015.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!