Simba Queens imefuzu kwenda Morocco kucheza fainali za CAF Champions League kwa soka la wanawake baada ya kuifunga She Corporate ya Uganda kwa goli 1-0 lililofungwa na Corazone kwa mkwaju wa penati dakika ya 49.
Mchezo huo wa fainali ya CECAFA Zone Qualifiers umeipa Simba Queens Ubingwa wa CECAFA kwa wanawake pamoja na kufuzu kwenda Morocco.
Michuano ya CAF Champions League kwa wanawake huwa inachezwa katika taifa moja ikijumuisha jumla ya timu 8, sita mabingwa kutoka zone sita za soka, nafasi mmoja ya Bingwa mtetezi na nyingine Bingwa wa nchi mwenyeji.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!