Makarani wa Sensa wameonywa kuacha tabia ya kupiga picha na kurekodi mahojiano yao na Watu pindi wanapokwenda kuwahesabu kwakuwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.
Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dr. Albina Chuwa akiwa Mkoani Iringa amesema kumekuwa na video zinazosambaa mitandaoni zikionesha Watu wanaofanyiwa mahojiano na Makarani katika kaya zao.
Dr.Chuwa amesema endapo Karani yoyote atakamatwa kwa kosa hilo kwa mujibu wa sheria atalipa faini ya Tsh. Milioni mbili au kwenda Jela miezi 6 au vyote viwili kwa pamoja.
Katika hatua nyingine Chuwa amewataka Wasimamizi wa Sensa ngazi zote kupita kaya kwa kaya kuhakiki zoezi la Sensa na kuhakikisha taarifa zilizotolewa na Makarani ni sahihi.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!