Kuongezeka theluji katika Mlima Kilimanjaro kumekuwa kivutio kwa
wananchi ambao baadhi wamekuwa wakipiga picha mandhari ya mlima huo.
Hata hivyo, baadhi wamekuwa wakihoji iwapo hali itaendelea kuwa hivyo.
Akizungumzia hali hiyo, Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za
Taifa Tanzania (Tanapa), Paschal Shelutete amesema hali hiyo inatokana
na mvua iliyonyesha Januari Mosi,2018.
Shelutete amesema leo Januari 3,2018 kuwa mvua inayonyesha kwenye uwanda
wa juu kuanzia mita 3,500 kutoka usawa wa bahari inakuwa katika mfumo
wa theluji.
Amesema hali hiyo inatokana na kiwango kidogo cha joto ambacho kwa usiku hufika hasi (sentigredi sifuri au chini).
“Theluji hii huyeyuka kukiwa na mabadiliko ya hali ya hewa hasa kiangazi
(kunapokuwa na jua). Upande mwingine kukiwepo na mvua endelevu na
mabadiliko ya hali ya jua na joto theluji huungana na kuwa barafu ya
kudumu,” amesema.
Mwongozaji watalii katika kampuni ya Zara Adventures Tours ambaye pia ni
mwenyekiti wa waongoza watalii katika Mlima Kilimanjaro na Meru,
Faustine Chombo amesema theluji imeongezeka lakini ni ya muda kutokana
na mvua iliyonyesha.
Amesema hali ya hewa katika Mlima Kilimanjaro kwa sasa ni ya mvua ndiyo
maana ukiuangalia mlima kutokea Moshi mjini unaonekana kuwa na theluji
nyingi.
Amesema wamejipanga kupanda miti kila mwaka katika maeneo ya hifadhi ya
Mlima Kilimanjaro ili kusaidia jitihada za kuulinda na kuuhifadhi.
Chombo amesema kuna haja ya wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro kuhamasishwa
kupanda miti kwa wingi katika maeneo ya hifadhi hiyo hatua
itakayosaidia theluji kuendelea kuwapo.
COMMENT AND SHARE....!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!