Mwishoni mwa mwaka jana na mwanzo wa mwaka huu kocha wa Manchester United amekuwa habari kubwa, wengi wanaona Jose Mourinho amekosa raha na mambo yanayoendelea EPL.
Inasemekana kwamba uhusiano wa Mourinho na CEO wa Manchester United Ed Woodward hauko vizuri na hii inatokana na Jose Mourinho kutokubaliana na sera za usajili ambazo anafanya Woodward.
Mbaya zaidi Woodward na Mourinho wamepishana kuhusu manunuzi ya beki Danny Rose ambaye ilitajwa kwamba anakaribia kutua United lakini Manchester wanaonekana kugoma kutoa pesa za kumnunua.
Inadaiwa pia kwamba Mourinho hakai tena Manchester kama zamani na muda wake mwingi huwa anautumia London ambako ndiko nyumba yake ilipo huku Manchester akiwa anaishi katika hoteli.
Kivuli cha Pep Gurdiola nacho kinatajwa kumsumbua sana Jose Mourinho kwani sasa inaonekana wazi kwamba Man City wanaelekea kubeba kombe la EPL jambo ambalo linamfanya Mou kujiona mnyonge.
Tayari PSG wameshatajwa kama sehemu ambayo Mourinho anaelekea, na tayari Mou anasema jiji la Paris ni mahala pazuri kuishi kwani alizisikia sifa za mji huo kutoka kwa mwanaye ambaye amewahi kukaa katika mji hio.
Waandishi wengi na wachambuzi wa masuala ya michezo nchini Uingereza wametabiri kwamba Jose hatakuwa na United katika msimu ujao wa ligi na kama United watakosa kombe msimu huu inaweza kumfanya Mou kubwaga manyanga.
COMMENT AND SHARE............!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!