Msanii kutoka Ufaransa Abraham
Poincheval anaendelea kutamia mayai ya kuku akiwa na matumaini kwamba
mwishowe yataangua vifaranga.
Msanii huyo anatumia joto kutoka kwa mwili wake kutamia mayao hayo 10.
Poincheval
ambaye hufanya uigizaji wa kuigiza mambo ya ucheshi lakini ya hatari
tayari ameishi wiki mbili ndani ya dubu, miongoni mwa mambo mengine ya
kushangaza.
Atakuwa katika chumba maalum ambacho anatamia mayai,
ambapo watalii wanaweza kumtazama katka makumbusho ya Palais de Tokyo
mjini Paris.
Anatarajia kutamia mayai hayo kwa siku 21 hadi 26.
"Kusema mweli, kimsingi, ni kama nimekuwa kuku," anasema.
Poincheval, 44, ameuita uigizaji huo wake - "Oeuf" (Yai kwa Kifaransa).
Badala
ya kutamia mayai hayo kwa kuchutuma juu yake moja kwa moja, anatumia
kiti maalum ambacho kina mfuko eneo lake la kukalia. Hapo ndipo mayai
hayo yamewekwa.
Poincheval atakuwa amejifunga blanketi kuzuia joto kupotea.
Aidha, anapanga kula vyakula vinavyoongeza sana joto mwiliki, kama vile tangawizi.
Wakati wa haja, atatumia kijisanduku kidogo kilichomo mvunguni mwa kiti chake.
Ndipo mayai hayo yaangue vifaranga, hahitaji kuondoka zaidi ya dakika 30 kwa siku. Anapanga kutumia muda huo kula chakula.
Uigizaji wa sasa wa Poincheval anaufanya baada ya uigizaji wake
aliouita "Pierre" (Jiwe kwa Kifaransa), ambapo aliishi ndani ya jiwe
kubwa lililokuwa limechongwa sehemu ya kutoshea mwili wake ndani.
COMMENT AND SHARE..............................!!!!!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!