Wanasayansi wamethibitisha kuwa mitandao ya kijamii ndicho chanzo cha
magonjwa mbalimbali yakiwamo ya akili na kulemaa kwa mishipa ya shingo.
Wanasayansi wanaeleza kuwa mitandao ya kijamii kama vile facebook,
twitter, whatsApp na instagram, ujumbe wa simu na michezo ya kwenye
intaneti husababisha magonjwa ya akili, uraibu na kujeruhiwa kwa shingo
na uti wa mgongo kunakosababishwa na kuinamia simu muda mrefu.
Tovuti ya Neck Institute (London) imeeleza kuwa madhara ya shingo na uti
wa mgongo yanayosababishwa na matumizi ya simu kwa muda mrefu hasa kwa
kuandika ujumbe mfupi au Text Neck Syndrome, huathiri mamilioni ya watu
duniani.
Daktari bingwa wa neva za fahamu (neurologist) wa Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili, Profesa William Matuja amesema bado hakuna ushahidi wa
kisayansi kama matumizi ya simu yanaathiri mishipa ya shingo, lakini
namna ya matumizi yake yalivyo yanaathiri misuli.
Profesa Matuja amesema kuinamia simu muda mrefu kunasababisha maumivu ya mgongo, shingo na hata kichwa.
Daktari wa mishipa ya fahamu, wa Florida nchini Marekani, Dean Fishman
amesema mishipa ya shingo hasa kwa sehemu ya nyuma huathirika kutokana
na kuandika ujumbe mfupi kila mara na kwa muda mrefu, kwa sababu kitendo
hicho kinamfanya mtumiaji kuiinamia simu.
COMMENT AND SHARE.............................!!!!!!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!