BAADA ya Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk. Harrison
George Mwakyembe kutamka hadharani kuwa na mipango ya kuwapatanisha
wakali wa Muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Ali
Saleh Kiba ‘King Kiba’, sababu sita zitakazomfanya waziri huyo kugonga
mwamba, zimeelezwa IMEKUJAJE?
Hivi karibuni Waziri Mwakyembe akiwa mkoani Dodoma alizungumza na
waandishi wa habari akitoa wito kwa Watanzania kuichangia Timu ya Taifa
ya Vijana Chini ya Miaka 17 (Serengeti Boys) huku akitaja listi ya wadau
mbalimbali wanaoongoza hamasa hiyo.
Miongoni mwa watu aliowapongeza walikuwa ni Diamond na Kiba na kusema
kuwa, amefurahishwa kuwepo kwao katika hamasa hiyo na kuwataka kukutana
nao Dodoma mara moja kwani anasikia kuwa hawakai pamoja na kuongeza
kwamba, yeye ni kama baba yao hivyo lazima watakaa pamoja (kuelewana).
Kutokana na tamko hilo, vyanzo vya karibu na wakali hao, vimetonya kuwa,
jambo hilo haliwezekani huku sababu sita (6) zitakazomfanya Waziri
Mwakyembe kugonga mwamba;
SABABU YA KWANZA
Mmoja wa vyanzo vya karibu na wawili hao, alitoa sababu ya kwanza kuwa
ni kujitengenezea fedha. Kwamba kuendelea kuwa na bifu kutawafanya
kuendelea kuwa na ushindani hivyo ni jambo lililokaa kibiashara hivyo
hawapo tayari kupoteza fursa hiyo.
“Hivi karibuni Diamond alifungua tovuti ya Wasafi.com ambayo imekusanya
karibu nusu ya wasanii wa muziki wakubwa nchini, wanauza kazi zao huko
kwa makubaliano na fedha kidogo zinaingia kwake nyingine kwa wasanii
hao. Diamond amekuwa akitamka kuwa anapenda na Kiba ajiunge nao.
“Kiba naye amekuwa mgumu wa kukubali kwa maana ameshaona kuwa kupeleka
nyimbo zake Wasafi. com, kwanza kutaliua bifu lao linalomsaidia vitu
vingi vya faida na pili atakuwa chini ya Diamond ambapo atakuwa kama
anamtengenezea fedha mtu ambaye anashindana naye kwenye biashara ya
muziki.
Kutokana na tamko hilo, vyanzo vya karibu na wakali hao, vimetonya kuwa,
jambo hilo haliwezekani huku sababu sita (6) zitakazomfanya Waziri
Mwakyembe kugonga mwamba;
SABABU YA PILI
Chanzo hicho kilizidi kutiririka kuwa, sababu ya pili itakayomfanya
Waziri Mwakyembe kugonga mwamba ni mameneja wa wasanii hao
kutoshirikiana kwa ukaribu.
“Tangu nimemfahamu Diamond akiwa chini ya Babu Tale na Sallam SK
sijawahi hata siku moja kuwaona kwenye meza moja wakitafuta suluhu na
meneja wa Kiba, Seven.
Hawajawahi hata kushirikiana wala kuandaa shoo ya pamoja na inapotokea
shoo wakapangiwa pamoja lazima mmojawapo atakataa au kuweka masharti
magumu au kufanyiana fitina.
“Ipo mifano mingi inayoonesha wazi hawaivi chungu kimoja. Kama
utakumbuka katika Tamasha la Rock lililofanyika Viwanja vya Golf,
Mombasa mwaka jana likimshirikisha staa kutoka Marekani, Christopher
Maurice ‘Chris Brown’, Kiba naye alikuwa mgeni mwalikwa ambaye alipafomu
lakini liligeuka kuwa na sintofahamu baada ya Kiba kupanda na kupafomu
nyimbo mbili tu, ikiwemo Mac Muga kisha kuzimiwa kipaza sauti na baada
ya kushuka malalamiko aliyaelekeza kwa Meneja wa Diamond, Sallam kuwa
amefanya yote hayo,” kilisema chanzo hicho.
SABABU YA TATU
Sababu ya tatu inaelezwa kuwa ni kukwepana wasanii hao kwa muda mrefu
pindi wanapoandaliwa matamasha au linapotokea jambo la kuwakutanisha.
“Kwa muda mrefu Kiba na Diamond wamekuwa wakikwepana na ukweli huu upo
wazi kwa mashabiki wao. Walishawahi kukwepana mwaka 2015 katika Viwanja
vya Leaders jijini Dar katika moja ya shoo iliyoandaliwa na Kampuni ya
Mawasiliano ya Tigo ikitambulika kama Tigo Kiboko Yao ambapo Kiba
hakutumia mlango maalum wa VIP (aliruka fensi) kuingia ndani kwenye eneo
la wasanii wenzake akiwemo Diamond.
“Mwaka jana katika sherehe ya kutimiza miaka 10 ya Chama cha Orange for
Democratic Movements (ODM) cha Raila Odinga, Kiba na Diamond walialikwa
bila kujuana katika Viwanja vya Mama Ngina, Mombasa kutokana na
kutokuelewana kwao. Kilichotokea usiku huo, Diamond alitangazwa kama
msanii rasmi atakayetumbuiza akafanya hivyo na baada ya hapo Kiba naye
aliingia kama msanii wa sapraizi, jambo lililofanya shangwe kuzidiana na
kuonekana kama mmoja amefunikwa,” kilisema chanzo chetu.
SABABU YA NNE
Chanzo kingine cha karibu na wasanii hao kiliongeza kuwa sababu nyingine
ambayo ni ngumu kwa waziri huyo kuwapatanisha ni kila mmoja kutaka
kuendelea kuwa kileleni. “Diamond ni msanii mkubwa sawa na Kiba,
kumekuwa na ushindani sana kila mmoja kuendelea kukaa kileleni kwa kutoa
nyimbo kali, ndiyo maana umesikia Kiba amesainiwa na Sony Music Africa
na wakati
huohuo Diamond naye ameingia saini na Lebo ya Universal Music Group
kusambaza kazi zake na za lebo yake,” kilisema chanzo hicho ambacho ni
mchambuzi wa masuala ya burudani na mastaa Bongo.
SABABU YA TANO Ilifahamika kuwa, sababu nyingine kubwa inayoleta
ugumu wa wawili hao kupatana ni kuundwa kwa timu (team) ambazo zimekuwa
zikigandamizana kimuziki. Kiba ana team yake (Team Kiba) na Diamond
(Team Diamond). “Team zote hizi zimekuwa zikilikoleza bifu la Diamond na
Kiba na kufanya kuwa ngumu kupatana.
Kama kweli waziri anataka kuwapatanisha, angeanza kudili na makundi
haya. Mfano inapotokea Diamond akapata tuzo au akafanya vizuri sehemu
f’lan ni wazi timu hizi zitaanza kupondana. Inasemekana kuwa, imefikia
hatua hata wawili hao wanapochaguliwa katika tuzo za kimataifa wakiwa
kipengele kimoja au mmojawapo akichaguliwa kushiriki basi hizi timu
hushirikiana kuuangusha upande wa pili,” kiliendelea chanzo hicho.
SABABU YA SITA Sababu ya sita na ya mwisho iliyotajwa kuleta
ugumu wa kuwapatanisha wawili hao ni kutokuwa tayari. Kila mmoja kwa
upande wake akihojiwa husema kuwa hana tatizo na mwenzake japokuwa kuna
kinyongo wamejiwekea.
“Diamond na Kiba wenyewe hawajawa na utayari wa kupatana. Ukikaa na Kiba
atakuambia hana bifu naye na Diamond vivyohivyo. Ujue hawa wana
kinyongo tangu wafutiane nyimbo. Diamond alimfuta Kiba katika Wimbo wa
Lala Salama na Kiba naye akalipiza kumfuta katika Wimbo wa Single Boy,”
kilimaliza chanzo.
MTAZAMO WA DULLY Kuhusu kupatana kwa Diamond na Kiba, staa ambaye
ni mkongwe katika Bongo Fleva, Dully Sykes alikaririwa akisema kuwa,
kwa sasa wasanii hao kupatana ni jambo gumu mpaka atakapotokea msanii
atakayewazidi na kuwa kileleni kwa kila kitu zaidi yao.
COMMENT AND SHARE.......................................!!!!!!!!!!!!!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!