Ngono kinyume na maumbile au wengine husema Ngono kwa nyia ya haja
kubwa, ni hali ya kingono ambayo muhusika huingiza uume katika njia ya
haja kubwa kwa lengo la kufanya mapenzi kwa njia hiyo ili kujirishiza
hisia zake.
Watu ambao wanajishughulisha na kushiriki katika ngono ya nia hii ya
kinyume na maumbile wapo katika hatari kubwa ya kiafya, kwa sababu njia
ya haja kubwa inazungukwa na mishipa/neva nyingi sana zipo eneo hilo
ambalo kazi zake si maalumu kwa tengo la ngono kwa kuingiziwa kitu
ambacho hakistahiri eneo hilo.
Ambapo kwa utafiti uliofanyika Nchini Tanzania uliohusisha wasichana na
wanawake wa rika kuanzia miakan 15 na kuendelea na iliyohusisha kada
tofauti katika jamii kama wanafuzi, wafanyakazi, wahudumu wa baa,
wauguzi, makahaba na kina mama wa majumbani katika maeneo tofauti. Watu
waliojitokeza ni 903 wakiwemo pia wanaume walihusika katika tafiti hiyo.
Utafiti huo ulisema wanawake 44 kati ya 166 waliohojiwa walisema kuwa
wamewahi kufanya tendo la kujamiiana kinyume na maumbile ambao ni sawa
na asilimia 27 huku asilimia 73 ya waliohojiwa walidai kufahamu njia
hiyo ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile, katika Utafiti huo
ulifanywa na Irene Mremi kutoka Taasisi ya utafiti wa magonjwa ya
binadamu Nchini Tanzania.
Inakadiriwa kuwa asilimia 90% ya wanaume wanaofanya ngono na wanaume
wenzao (mashoga) huwa wanajihusisha na ngono kinyume na maumbile.
JE, NGONO KINYUME NA MAUMBILE NI SALAMA?
HAPANA, Ngono kinyume na maumbile si salama kwa sababu ina madhara mengi kiafya kama yafuatavyo;
MOJA, Njia ya haja kubwa haina vilainishi/lubrication asilia kama jinsi Uke ulivyo.
Hivyo wakati wa tendo la ngono husasani wakati wa uingizaji wa uume huwa
inasababisha kuchubuka kwa tisu/ngozi laini ndani ya njia ya haja kubwa
hiyo, na hivyo kupelekea michubuko ambayo bacteria, virusi na hata
vimelea vingine kuweza kupenyea wakati wa majeraha hayo ya michubuko na
hivyo kuingia katika mfumo wa damu kupitia majeraha hayo.Hii inaweza
kusababisha kuenea kwa magonjwa ya zinaa pamoja na VVU.
Tafiti zinaonyesha ya kuwa Ngono kwa Njia ya haja kubwa ipo katika
hatari kubwa ya maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa zaidi ya asilimia
30% kuliko watu wanaotumia njia ngono kwa njia ya Uke.
Vile vile mtu anakuwa katika hatari kubwa ya kupata virusi vya human
papillomavirus (HPV ) ambavyo huweza kumpelekea mtu anayejihusisha na
ngono kinyume na maumbile kupata muwasho katika eneo hilo la haja kubwa
na hata kupelekea kupata kansa.
PILI, Tishu ndani ya njia ya haja kubwa, haijakingwa na kulindwa kwa
ngozi ngumu kama ilivyo sehemu za nje za mwili. Tishu zote za nje ya
miili yetu zina ngozi ambayo ni seli zilizokufa ambazo hutusaidia
kutukinga dhidi ya maabukizi ya vimelea na vile vile hutulinda na vitu
tofauti katika mazingira.
Hivyo ndani ya njia ya haja kubwa hakujakingwa na ulizi huo wa asili wa
seli hizo ili kuweza kuhimili, hivyo kuifanya iwe katika hatari kubwa ya
kusuguliwa na hivyo kuchanika ambayo hupekea kusababisha maambukizi
kuwa rahisi kutokea.
Pia ngozi ndani ya njia ya haja kubwa iko tofauti na ile ya ukeni ambapo
ngozi ya ukeni huweza kuhimili ile misuguano pasipo kuweza kusababisha
michumbuko kwa sababu ya vilainishi asili vinavyoatikana ndian ya uke na
gozi husika.
TATU, Njia ya haya kubwa ni Maalumu kupitisha Kinyesi tu.
Kwa jinsi ambavyo njia hii imeundwa ama kutengenezwa ni maalumu kwa kuhimili na kupitisha kinyeshi tu na si vinginevyo.
Njia ya haja kubwa imezungukwa na kama misuli mfano wa ringi ama kwa
kitaalamu huitwa (Anal sphincter) ambayo kazi yake ni kukaza eneo hilo
kabla na baada ya kujisaidia tu.
Kipindi ambapo misuli hiyo (anal sphincter)imekazwa ama kubwa kwa
kuingiziwa kitu kingine kigumu huweza kusababisha maumivu makali kwa
muhusika.
Panapoendelea kuwa na mrudio wa mara kwa mara wa ufanyaji wa Ngono kwa
njia hii ya haja kubwa ama kinyume na maumbile hufanya misuli hiyo ya
njia ya haja kubwa kuwa dhaifu ama kulegea na isiwe na uwezo tena
wakukaza kama kazi yake inavyotakiwa kufanya. Na hivyo kuwa vigumu
kuweza kuzuia kinyesi kuweza kupita mpaka utapokuwa tayari kuweza
kukitoa hivyo kusababisha utokaji ovyo wa kinyesi.
NNE, Njia ya haja kubwa imejaa bacteria wengi.
Njia ya haja kubwa imejaa bacteria wengi sana tofauti na Ukeni kulivyo
hata kama wapenzi hawana maambukizi yeyote ya zinaa au ugonjwa wowote
bacteria huwa wapo tu eneo hilo na hawa ni bacteria wa kawaida (Normal
flora).
Mtu anapokuwa naingiza uume ndani ya njia ya haja kuwa anakuwa anaingiza
vimelea vingine vya bacteria katika eneo hilo na wanapokutana na wale
bacteria wengine waliopo katika eneo hilo husababisha madhara.
Pia pale unapohamisha uume toka katika njia ya haja kubwa na kupeleka
katika Njia ya Uke badi bacteria hao utawapeleka katika eneo Uke ambapo
Njia ya haja kubwa inakuwa na bacteria wengi na hivyo kupelekea
maambukizi ukeni na pia maambukizi katika njia mkojo.
Ngono kwa njia ya haja kubwa inaweza kusababisha madhara mengine kwa
afya ya watu wanaojihusisha na Njia hii ya ngono na wanaweza kupata
madhaara kama haya yafuatayo,
Pale mdomo unapogusana na njia ya haja kubwa au kugusa uume uliotoka
kwenye njia ya haja kuwa kwa mdomo kunaweza kupelekea kupata kwa wote
mtu na mpenzi wake kuwa katika hatari ya kupataa magonjwa ya HEPATITIS
C, HERPES/ malengelenge, kupata virusi vya human papillomavirus (HPV) na
maambukizo mengine.
Hata hivyo, majeraha makubwa wakati wa ngono kwa njia ya haja kubwa mara
nyingine ingawa sio kila mara hali hii kutokea inaweza kupelekea Damu
kuvuja kwa ndani (hemorrhoids) baada ya tendo hilo kufanyika ambalo
inaweza kusababisha au kupasuka ama kuchanika kwa misuli/nyama ndani ya
njia ya haya kubwa kwa sababu ya msuguano mkali na muda mwingine
hupelekea kuweza kutoboka kwa utumbo mpana(colon) hii huweza kwa ni
tukio la hatari zaidi ambalo huhitaji msaada wa kitabibu haraka kwa
matibabu na hata kufanyiwa upasuaji zaidi na hata kupoteza maisha
kunaweza kutokea.
TANO, pia kwa wanawake wengi wanaofanya ngono kinyume na maumbile
wamekuwa wakipata shida wakati wa kujifungua kwa misuli yao kushindwa
kuhimili kukaza kwakati wa kusukuma mtoto na hivyo inaweza kupelekea
utokaji wa kinyesi wakati wa kusukuma mtoto. jambo ambalo huleta tabu
kwa wahudumu wa afya kwa kutumia muda mwigi kuwahudumia.
Njia pekee ya kuepuka kabisa hatari hizo za ngono kinyume na maumbile ni kuacha kabisa ngono kwa njia hiyo ya haja kubwa.
shiriki katika ngono kwa njia ya kawaida na ikibidi kwa kutumia kondomu
ili kujilinda dhidi ya kuenea kwa maambukizi ya magonjwa ya zinaa.
Kuepuka kuingiza uume ndani ya uke na kisha mdomoni ikiwa uume ulikuwa umeingizwa katika njia ya haja kubwa.
Ikiwa umepata michubuko na kutoka damu baada ya ngono ama vidonda
karibia na njia ya haja kubwa na hata katika maeneo ya uke basi onana na
daktari wako haraka iwezekanavyo ili upatiwe tiba hii iakusaidi kuzuia
maambukizi ya vimelea katika eneo la jeraha.
MADHARA ANAYOWEZA KUYAPATA MWANAUME ANAYEPENDA KUJIHUSISHA NA MCHEZO HUU WA NGONO NI KAMA IFUATAVYO;
KWANZA, Kunauwezekano wa Njia ya haja ndogo kuziba kiasi au kuziba
kabisa kwa sababu ya vimelea kuingia na kuziba ama kuingia kwa kinyesi
katika njia ya haja ndogo hivyo kukuweka katika wakati mgumu utapohitaji
kujisaidia haja ndogo.
PILI, unaweza kupata magonjwa ya saratani(kansa) ya tezi tezi Prostate gland.
TATU, Maambukizi ya Virusi vya ukimwi kwa sababu kuna uwezekano mkubwa
sana wa kupata maabukizi tofauti na kwenye njia ya Uke hii ni kutokana
na kuwa na uwezekano mkubwa wa kupata michubuko kiurahisi.
NNE, Kuathirika kisaikolojia hivyo mhusika kuandamwa na msongo wa mawazo kila wakati kujutia tendo hili baya.
Nina imanai ndugu msomaji wa makala hii umeweza kuona madhara mabaya
sana ya tabia hii mbaya. Inawezekana umezoea mchezo huo wa kuwaingilia
wenzako ama kuingiliwa kwa namna hiyo na kuona raha lakini umeziona
hasara zake, amabazo kwa hakika kama wewe ni mmoja wao, unatakiwa kuacha
mara moja kwa vile mwisho wake ni majuto na mateso.
Jiepushe kuiga mambo bila kujua hasara zake, pia usimtie mwenzako
majaribu kwa kumlazimisha kufanya kitendo hiki na wanaume kwa kigezo cha
kuachwa kwa lengo la kuwaingilia kinyume na maumbile kwa kuwatishia
kuwaacha kama watakataa.
Kipi bora kuharibiwa ama kuachwa? Jibu unalo mhusika!!
Kumbuka baada ya kuharibiwa thamani yako inashuka mbele ya jamii. Kasha
kupelekea kuingia katika msongo wa mawazo na mateso ya ugonjwa ama
magonjwa utakayoyapata baada ya kukubali kuingiliwa kinyume na maumbile.
UKWELI MCHEZO HUU UMEWAATHIRI SANA WANAWAKE NA WANAUME AMBAO WENGI WANAUJUTIA.
JIEPUSHE NA NGONO KINYUME NA MAUMBILE!!!!!
COMMENT AND SHARE...................................!!!!!!!!!!!!!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!