Takwimu zinaonesha kuwa kila mwaka duniani kote kunatokea wagonjwa wapya
wa saratani wanaokadiriwa kufikia milioni 14.1, na kati ya hao zaidi ya
wagonjwa milioni 8.2 hufariki dunia kutokana na ugonjwa wa saratani.
Takwimu hizo ni kwa mujibu wa Shirika za Kimataifa la Atomiki la Utafiti
wa Saratani (IARC) na Shirika la Afya Duniani ambazo zimetolewa leo
mjini Dodoma na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee,
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ikiwa kesho ni siku ya Saratani Duniani na
kusema kuwa kwa Tanzania tatizo la saratani limekuwa likiongezeka na
kukua kila mwaka.
Amesema nchini Tanzania kila mwaka wagonjwa wapya wapatao 50,000
hugundulika na saratani za aina mbalimbali na kati ya hao ni wagonjwa
5,000 sawa na asilimia 10 ya wagonjwa wote ndiyo wanaofanikiwa kufika
katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road ili kuweza kupata tiba, huku
asilimia 70 ya wagonjwa wanaobahatika kufika katika taasisi hiyo na
kupata huduma za tiba hufika wakiwa katika hatua za mwisho za ugonjwa.
Amesema tayari serikali imetoa shilingi bilioni tano kwa ajili ya
ununuzi wa mashine mpya za mionzi ambazo zitasaidia kutibu wagonjwa wa
saratani.
COMMENT AND SHARE............!!!!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!