Baada ya Klabu Bingwa ya Afrika
Mashariki na Kati, Azam FC, kuanza rasmi mazoezi jana jioni kujiandaa na
mchezo ujao dhidi ya Ndanda, daktari wa timu hiyo, Mwanandi Mwankemwa,
amezungumzia hali ya kiafya ya baadhi ya wachezaji waliokuwa majeruhi.
Wachezaji
wa Azam FC waliokuwa majeruhi ni nahodha John Bocco 'Adebayor', Stephan
Kingue waliopata majeraha ya misuli ya paja kwenye mchezo uliopita wa
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) dhidi ya Simba, ambao matajiri
hao walishinda bao 1-0 lililofungwa na Bocco.
Wengine wanaouguza
majeraha, ambao waliukosa mchezo huo ni kiungo Salum Abubakar 'Sure
Boy', kipa Mwadini Ally (nyama za paja) na beki Shomari Kapombe, ambaye
ni mgonjwa lakini hivi sasa akiendelea vema.
Akizungumza na
mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz mara baada ya mazoezi ya jana,
Mwankemwa alisema kuwa Bocco na Kingue watakaa nje ya dimba kwa muda wa
wiki mbili tokea jana, huku Sure Boy akitarajiwa kuanza rasmi mazoezi
leo na Mwadini akipumzishwa kwa siku tatu kuanzia jana.
"Bocco
hali yake inaonekana kuimarika vizuri tokea alipopata majeraha hayo ya
kuchana msuli wa nyuma ya paja, Stephan (Kingue) kwa upande wake naye
amechana msuli wa mbele ya paja, hivyo wote watakaa nje ya dimba kwa
muda wa wiki mbili kutoka sasa (jana) na wataanza mazoezi mepesi baada
ya wiki moja," alisema.
Daktari huyo bingwa mzoefu, alisema hali
za wachezaji wengine ziko vizuri kabisa kuenndelea na mikikimikiki ya
maandalizi kuelekea mechi zijazo za ligi pamoja na michuano mingine.
COMMENT AND SHARE.....................!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!