Mjomba wake mshambuliaji wa
Liverpool Sadio Mane, anasema kuwa anahofia usalama wa familia yake
baada ya mpwa wake kukosa penalty na kusababisha Senegal kutimuliwa
kutoka mechi ya robo fainali wakati wa mashindano ya Afcon.
Sana
Toure alisema kuwa gari ambalo alikuwa amenunuliwa na mpwa wake Mane,
ambaye ndiye mchezaji ghali zaidi barani Afrika, liliharibiwa na nyumba
yake kulengwa.
"Siku baada la Lions kuondolewa, baadhi ya watu walio na nia mbaya
wakataka kuvamia nyumba yangu iliyo Malika. Nawashukuru majirani na
wenyeji, kitu kibaya kilizuiwa," Sana Toure alivyambia vyombo vya
habari.
Sadio Mane anaonekana kusahau yaliyomsibu Afcom na kufunga mara mbili Liverpool ilipokutana na Tottebnham wikendi hii.
COMMENT AND SHARE.................................!!!!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!