Mume wa msanii wa filamu za Kibongo, Shamsa Ford waliyefunga ndoa hivi
karibuni, Chid Mapenzi ametajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul
Makonda kwamba ni miongoni mwa watu wanaotuhumiwa kujihusisha na
matumizi ya madawa ya kulevya na kuagiza akakamatwe na polisi haraka
iwezekanavyo.
Makonda ameyasema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari,
uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere, Posta jijini
Dar ambapo ametangaza kwamba anayo orodha nyingine ya watu 97
wanaotuhumiwa kuhusika na biashara ya madawa ya kulevya.
Pia mtu mwingine aliyetajwa ni Ayubu Mfaume ambapo naye anatakiwa kukamatwa haraka iwezekanavyo.
COMMENT AND SHARE................................!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!