
Msanii Rehema Chalamila a.k.a Ray C ambaye ametamba kwenye anga la Bongo
Fleva kwa siku nyingi, ameweka wazi kuwa kwa sasa hayuko kwenye
mahusiano ya kimapenzi na mwanaume yeyote.
Ray
C ambaye amerejea kwenye game kwa kasi baada ya kutoka kwenye dimbwi ya
matumizi ya dawa la kulevya hakutaka kueleza sababu za kuamua kuishi bila
mpenzi.
Msanii huyo aliyewahi kutikisa na ngoma kadhaa za bongo fleva
zenye ujumbe wa mahaba kama vile Wanifuatia nini, Na wewe milele
n.k atatikisa jukwaa la Azura Jumanne katika usiku wa Valentine, ambapo
amesema amepania kutoa burudani kali kutokana na kukaa muda mrefu bila
kufanya show,
Ameahidi kukata kiu ya wote waliokuwa wamem-miss huku akiwataka kufika ukumbini hapo na wapenzi wao "Mimi
ni mtu wa mapenzi, nimetayarisha nyimbo nzuri, sijafanya show muda
mrefu, nitaimba nyimbo zangu kadhaa, na nawashauri kila mtu aje na
mpenzi wake, ndiyo Valentine itanoga, pia kutakuwa na kila aina ya
burudani pamoja na dinner"
Kuhusu kurudi, amesema ana hamu ya
kurudi kwenye game na tayari amesharekodi nyimbo kadhaa, lakini
alishauriwa aanze na Valentine kwanza
"Naendelea kurekodi, bosi wangu alinishauri nifanye kwanza kwa ajili ya Valentine maana watu wanaulizia sana"
KUHUSU RECHO
Katika hatua nyingine,
Ray C alitakiwa kutoa maoni yake kuhusu Msanii Recho ambaye amekuwa
akifuata nyayo zake kuhusu kutajwa kwake kwenye orodha ya watu
wanaohusika na dawa za kulevya, lakini alisema hawezi kuzungumzia suala
hilo kwa kuwa hana uhakika juu ya suala hilo
"Mimi Recho namjua vizuri,
lakini kutokana na matatizo yangu sijaonana naye muda mrefu sana, sipo
hapa kumzunguzia mtu, na siyo vizuri, pia siyo vizuri kuzungumzia kitu
ambacho sina uhakika nacho maana mimi sijawahi kumuona akitumia hiyo
kitu. Nachoweza kusema ni kuwa kama mimi niliweza, kila mtu anaweza,
naamini atakuwa poa maana najua ni mwanamke imara" Amesema Ray C
COMMENT AND SHARE................................!!!!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!