SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) inakusudia kutunga sheria ya
kuzuia uvutaji wa sigara hadharani katika visiwa vya Unguja na Pemba.
Hatua hiyo ilitangazwa jana na Waziri wa Afya, Mahmoud Thabit Kombo,
wakati akijibu swali la Mwakilishi wa Mpendae kwenye Baraza la
Wawakilishi.
Mwakilishi huyo, Mohammed Said Dimwa, alitaka kujua athari kubwa
inayopatikana kutokana na utumiaji wa sigara pamoja na mikakati ya
wizara katika kukabiliana na hali hiyo.
Waziri huyo alisema serikali imeamua kuchukua hatua hiyo kutokana na
uwapo wa idadi kubwa ya wagonjwa wa maradhi yasiyoambukiza na kwamba
uvutaji wa sigara umebainika kuwa chanzo chake.
Kombo alisema katika kukabiliana na hali hiyo, Serikali itatenga maeneo maalum ya uvutaji wa sigara.
COMMENT AND SHARE............................!!!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!