Meneja wa Chelsea Antonio Conte
anasema hapendi mzaha wa meneja wa Manchester United Jose Mourinho,
baada ya Mourinho kusema kuwa Chelsea hucheza mchezo wa kujilinda tu.
Chelsea iko kileleni na pointi 10 baada ya mechi ya Jumapili ambapo walitoka sare ya bao moja na Burnley.
Mourinho
ambaye anafahamika kwa kuwafanyia mzaha mahasimu wake, alisema kuwa
klabu hiyo yake ya zamani haiwezi kuimarisha mchezo wao kwa sababu wao
hushinda kwa kujibu mashambulizi.
Mourinho alikuwa akiongea baada
ya Manchester United kuwashinda Watford mabao 2-0 siku ya Jumamosi na
kuweka rekodi yao ta kutoshindwa hadi mechi 16. Man U wako nafasi ya
sita katika jedwali la ligi pointi 12 nyuma ya Chelsea.
COMMENT AND SHARE................................!!!!!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!