Uzazi wa mpango una mambo mengi sana.. sio kuzuia mimba tu ndio uzazi wa
mpango ila hata kupanga idadi na jinsia za watoto ni moja ya njia za
uzazi wa mpango..
Watu wengi wamekua wakitamani jinsia flani za watoto ili wazae watoto
wachache ila kukosa kwa jinsia waliyoipanga hujikuta wakizaa watoto
wengi wakati wakitafuta jinsia husika, mpaka familia hugombana na
kutengana kwa sababu hizi.
Mara nyingi wazazi wa kiume hufikia hatua ya kuvunja ndoa kabisa hasa wanapokosa watoto wa kiume.
Leo ntamaliza kitendawili hiki kwa kutoa njia ambazo zinaweza kufanya mtu kupata mtoto wa kiume kwa asilimia nyingi…
Kitaalamu mbegu zinazotoa mtoto wa kiume XY huenda kwa mwendo mkali
sana kwenda kwenye mfuko wa uzazi lakini hufa haraka. lakini mbegu
zinazotoa mtoto wa kike XX husafiri taratibu na huchelewa kufika na kufa
ndani ya mfuko wa uzazi kwani mbegu hizi huweza kuvumilia hali mbaya
ya kimazingira ndani ya mfuko wa uzazi wa mwanamke, hivyo njia pekee ya
kupata mtoto wa kiume ni kuhakikisha mbegu hizo za kiumeXY zinakutana na
mayai ya kike kwenye mfuko wa uzazi haraka kabla ya kufa..
Zifuatazo ni njia hizo tano kali…
1. Hakikisha unashiriki tendo la ndoa siku mayai ya mwanamke yanapokua yameshuka{ovulation}
Ukishiriki tendo la ndoa siku hii ambayo yai linakua limeshuka
mbegu za kiume huweza kufika mapema na kujiunga na mayai ya kike na
kutengeneza mtoto{fertilization}hii ni siku ya 14 KABLA YA KUONA DAMU YA
MWEZI UNAOFUATA SIO BAADA YA KUONA SIKU ZAKO..
Kama wewe mwanamke hujui siku yako ya ovulation fanya hivi.
Pima joto lako la mwili: nunua kipima joto[thermometer} na kisha pima
joto lako kila asubuhi , siku ukiona joto lako limeongezeka kidogo ujue
umeanza ovulation na hiyo ndio siku muhimu ya kutafuta mtoto..
Angalia maji maji ya uke: kawaida maji ya uke hua mazito na
kuvutika kama maji ya mayai mabichi wakati mwanamke anapoanza
ovulation..
2. Wewe mwanaume ongeza idadi ya mbegu zako..{sperm count}
Mwanaume anatakiwa aongeze wingi wa mbegu zake hasa kwa kukaa siku mbili
mpaka tano bila kushiriki tendo la ndoa wakati akisubiri mwanamke wake
aanze ovulation.
Njia zingine za kuongeza mbegu ni
a) weka korodani kwenye hali ya ubaridi:
kawaida korodani hutengeneza mbegu nyingi wakati wa hali ya ubaridi
kuliko joto hivyo mwanaume anatakiwa kuepuka kuvaa nguo zilizobana
sana, na kuwekalaptop kwenye mapaja
b) acha kuvuta sigara na kunywa pombe:wanaume wanaokunywa pombe na
kuvuta sigara hua na mbegu kidogo sawasawa na wavutaji wa bangi..
matumizi ya dawa za cancer pia husababisha uzalishaji wa mbegu kidogo sana.
3. Tumia style za ngono ambazo zinahamasisha muingilio mkubwa{deep penetration}
Hii huzipa faida mbegu za mtoto wa kiume{XY} kufika haraka na kufanya
fertilization na upande mwingine, muingiliano mdogo{shallow
penetration}husababisha mbegu kumwagwa mbali na mlango wa mfuko wa uzazi
hivyo mbegu huweza kukutana na hali ya tindikali kwenye uke hivyo mbegu
za mtoto wa kiume kufa haraka na kuziacha mbegu zinazotoa mtoto wa
kike.{XX}.
4. Hakikisha mwanamke anafika kileleni:
Mwanamke anapofika kileleni hutoa maji mengi ukeni ambayo hupunguza
wingi wa tindikali ambayo ni adui wa mbegu zote hasa mbegu za mtoto wa
kiume XY ambazo hua haziwezi kuvumilia hali ngumu ya kimazingira.
5. Usifanye tendo la ndoa kabla na baada ya ovulation;
Kabla ya ovulation mbegu za mtoto wa kiume XY hufika haraka kwenye mfuko
wa uzazi kama kawaida na kukuta mayai ya mwanamke hayajafika na kufa
vivo hivyo baada ya ovulation..
COMMENT AND SHARE............................!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!