HABARI zilizotufikia hivi punde zimeelza kuwa wachimbaji sita wa madini
wanadaiwa kufukiwa na kifusi walipokuwa wakichimba madini kwenye mgodi
wa Buhemba ulioko mkoani Mara.
Imeelezwa pia kuwa watu 11 wamejeruhiwa kwenye ajali hiyo ambapo wamekimbizwa katika Hospitali ya Butiama kwa ajili ya matibabu.
Global Publishers imefanya jitihada za kumtafuta Kamanda wa Polisi wa
Mkoa wa Mara, Ramadhani Ng’anzi ambaye amekiri kutokea kwa ajali hiyo.
“Ni kweli ajali hiyo imetokea leo, na hivi sasa nipo eneo la tukio.
Kuhusu takwimu sahihi za watu waliofukiwa kwa sasa sina, mpaka uchunguzi
wa jeshi la polisi utakapofanyika ndipo nitatoa ripoti kamili.” Alisema
Kamanda Ng’anzi.
Tukio hilo ni la pili ndani ya kipindi kifupi ambapo siku za hivi
karibuni, wachimbaji 15 walifukiwa na kifusi na kuokolewa baada ya siku
kadhaa katika Mgodi wa RZ, Nyarugusu uliopo Nyarugusu mkoani Geita.
COMMENT AND SHARE................................!!!!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!