
Bingwa wa dunia wa mkanda wa WBO uzito wa welterweight, Manny Pacquiao
amewaomba mashabiki wake wa kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter
kumchagulia bondia wa kupambana naye katika mchezo ujao.
Mabondia hao ni Amir Khan na Kell Brook, wa Uingereza, Jeff Horn wa Australia na Terence Crawford, wa Marekani.
Pacquiao amesema pambano hilo la kutetea
mkanda ambao alishinda katika mwezi wa Novemba mwaka uliopita,
litafanyika katika nchi za falme za kiarabu.
Mfilipino huyo mwenye umri wa miaka 38,
na bingwa mara 6 wa dunia, alitangaza kustaafu katika mwezi wa Aprili,
mwaka uliopita, lakini alirejea tena ulingoni na kumshinda Jessie
Vargas mwezi wa Novemba, mwaka jana.
COMMENT AND SHARE..............................!!!!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!