
Mtu mmoja mwanaume ambaye hakufahamika jina, ameauwa kwa tuhuma za wizi
wa mlango, katika mtaa wa Mahina – Kanyerere Kata ya Butimba Wilayani
Nyamagana jijini Mwanza
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mwanza DCP Ahmed Msangi amesema kuwa tukio hilo
limetokea tarehe 13.02.2017 majira ya saa saa 8:45 ambapo mtu huyo
anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 25 hadi 30, aliuawa kwa kupigwa mawe
na fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake hadi kufariki dunia na kundi
la watu waliojichukulia sheria mkononi kwa tuhuma ya wizi wa mlango wa
mbao mali ya Filbert Nkwelo.
Inadaiwa kuwa marehemu alivunja dirisha
la wavu la nyumba ya Filbert Nkwelo na kuingia ndani na kuiba mlango
kisha wakati anatoka nje ili aondoke watu/wananchi walimuona na kuanza
kupiga yowe ya mwizi ambapo kundi kubwa la watu wakiwa na mawe na fimbo
lilimvamia na kumpiga sehemu mbalimbali hadi kufariki dunia.
Taarifa hiyo ya polisi imesema kuwa
hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kuhusiana na kifo hicho na kwamba askari
wanaendelea na upelelezi pamoja na uchunguzi kuhusiana na mauaji hayo.
COMMENT AND SHARE.................................!!!!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!