Zlatan Ibramovich Aipa Ubingwa Man United kwa Masharti..:;
on
Get link
Facebook
X
Pinterest
Email
Other Apps
Wakati United ikijianda kuivaa Liverpool leo saa moja
jioni, mshambuliaji wake mwenye maajabu Ibra Magic raia wa Sweden Zlatan
Ibrahimovic amesisitiza kuwa Manchester United bado inaweza kutwaa
ubingwa Ligi Kuu Uingereza msimu huu.
Man United imehaha kuendeleza kiwango
bora katika hatua za awali msimu huu, lakini mashetani hao wekundu
wameshinda mechi tisa mfululizo katika michuano yote, sita zikiwa ni
Ligi Kuu.
Kikosi hicho cha Jose Mourinho bado kipo
katika nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi lakini wamepunguza pengo
la pointi dhidi ya vinara Chelsea hadi kufika pointi 10 na Ibrahimovic
anaamini timu yake inaweza kupambana kutwaa ubingwa wa ligi iwapo
wataifunga Liverpool katika uwanja wa Old Trafford siku ya leo.
"Ligi haitabiriki. Hakuna timu ambayo
unaweza kusema itashinda na ikafanya hivyo," Ibrahimovic alikiambia Sky
Sports News. "Chelsea imekuwa ikifanya vizuri, wanacheza mara moja kwa
wiki, wana hali nzuri na nguvu nyingi kila wanapocheza, lakini walikuwa
na wakati mgumu mwanzoni lakini walizinduka.
"Kama tutapanda pale na kuwasumbua, kila
timu ina kipindi chake cha mafanikio. tumekuwa na wakati mzuri,
tukishinda, tukipoteza na sasa tunashinda tena. Natumai tutaendelea
hivyo na tunasubiri wengine wafanye makosa.
"Jumapili ni fursa nyingine ya kuchukua
pointi kutoka nne bora. Kama tunaweza kuanza vita dhidi ya timu zilizo
kwenye nne bora, baada ya kupoteza pointi nyingi ambazo hatukupaswa
kuzikosa. Pengo limekuwa dogo sasa, na pointi hizo tunaweza kuanza
kuzichukua kwa Liverpool,"
Ibrahimovic ambaye alitua Old Trafford
kwa uhamisho huru amefunga magoli 18 katika michuano yote akiwa United,
ikiwa ni pamoja na magoli 13 ya ligi
COMMENT AND SHARE....................!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!