Zaidi ya watu milioni moja wa
Uingereza wamesaini barua ya kutoa shinikizo kwa serikali ya Uingereza
kusitisha ziara rasmi iliopangwa baadaye mwaka huu ya rais Donald
Trump.
Barua hiyo iliyoandikwa kufuatia agizo la rais Trump dhidi
ya wahamiaji, inaeleza kuwa kuja kwake kutamuaibisha Malkia Elizabeth.
Idadi
ya watu wanaoendelea kusaini kupinga Mwaliko wa Trump nchini Uingereza
inaendelea kuongezeka, tangu Marekani kuweka vikwazo dhidi ya wageni
hatua iliyozua ghadhabu kote duniani.
Waziri Mkuu Teresa May alitangaza muwaliko huo wakati akiwa ziarani Marekani.
Afisi
yake imesema japo haikubaliani na baadhi ya sera za Trump hata hivyo ni
vyema Uingereza kuwa na ushirikiano wa karibu na Marekani.
Kiongozi wa Upinzani Jeremy Corbyin ametaka Waziri Mkuu kuahirisha ziara hiyo.
Wengi wanaopinga wanasema ziara ya Trump nchini Uingereza itakua aibu kwa Ufalme.
Ziara rasmi za serikali Uingereza huambatana na mualiko kutoka kwa Malikia, ambae huwapokea viongozi wawili wa nchi kila mwaka.
Aiki
jana Rais Trump aliweka sheria kusitisha mpango wa kuwapokea wakimbizi
na hasa kuwapiga marufuku wakimbizi wote kutoka Syria na wengine kutoka
nchi saba zote zikiwa za kiisilamu.
Siyo mara ya kwanza kumekua na kampeini kumpiga Trump Uingereza.
Mwaka wa 2015 raia laki tano walisaini kutaka kiongozi huyo kupigwa marufuku Uingereza.
Kiongozi
wa zamani wa chama cha Labour Ed Millibard amesema yeye na mbunge
mwenzake ambae ni mzaliwa na Iraq Nadhim Zahawi wataitisha muswada wa
dharura bungeni kujadili maombi ya raia.
Alex Salmond ambe alikua
kiongozi wa Scotland amesema Trump hafai kupata muwaliko Uingereza,
kauli yake ikiungwa mkono na Meya wa jiji la London Sadiq Khan.
COMMENT AND SHARE................!!!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!