Razer walidai laptop hiyo ya skrini tatu waliyoipatia jina Project Valerie ni ya kwanza ya aina yake dunianiKampuni
ya Razer imetangaza kwamba mbili kati kompyuta mpakato maarufu kama
laptop ambazo zina skrini tatu badala ya moja ambazo zilikuwa zimeundwa
na kampuni hiyo zimeibiwa.Laptop
hizo za maonesho, ambazo sana zinawalenga watu wanaopenda michezo ya
kompyuta, ziliibiwa wakati wa maonesho ya teknolojia ya CES yaliyokuwa
yakifanyika mjini Las Vegas, Marekani.Kompyuta hizo zilionyeshwa hadharani kwa umma mara ya kwanza wakati wa maonesho hayo.Kampuni
ya Razer inasema ilikuwa imebeba kompyuta tatu za aina hiyo lakini
waligundua Jumapili kwamba laptop mbili kati ya hizo zilikuwa zimetoweka
kutoka kwenye kibanda cha kampuni hiyo siku ya Jumapili.Skrini
zote tatu za laptop hiyo, ambayo imetajwa kuwa ya kwanza ya aina yake
duniani, ni za kiwango cha kuonyesha pikzeli 4,000 (4k) na ni za ukubwa
wa inchi 17 (43cm).Skrini mbili huchomoza kila upande kutoka kwa skrini kubwa ya kati, moja kwa moja.Afisa mkuu mtendaji wa kampuni hiyo Min-Liang Tan amesema kisa hicho kinachukuliwa "kwa uzito sana".Msemaji
wa Razer amesema kampuni hiyo imeahidi kutoa $25,000 (£20,600) kwa
atakayetoa habari za kusaidia "kutambuliwa, kukamatwa na kuadhibiwa" kwa
waliohusika katika uhalifu huo."Maafisa wetu walifanya kazi kwa miezi mingi kuunda kompyuta hizi," Bw Tan alisema kupitia ukurasa wake rasmi wa Facebook."Huu ni udanganyifu, ni wivi na haujatufurahisha. Yeyote aliyefanya hivi bila shaka ni mtu mjanja sana."Msemaji
wa Chama cha Watumiaji wa Teknolojia, shirika linaoandaa maonesho ya
CES, ameambia BBC kwamba ni kweli kisa cha kuibiwa kwa laptop hizo mbili
kimeripotiwa
Razer, kampuni ambayo ina makao makuu yake California, ilianzishwa na mjasiriamali kutoka Singapore Min-Liang Tan.Ni kampuni inayosifika na kuheshimiwa sana katika tasnia ya michezo ya kompyuta.Mashabiki
wa michezo ya kompyuta duniani walikuwa wamefurahia sana habari za
kuzinduliwa kwa kompyuta hiyo mpya ya skrini tatu ambayo imepewa jina
Project Valerie.
COMMENT AND SHARE..........!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!