Waziri wa mazingira huko Burundi
Emmanuel Niyonkuru, amefariki baada ya kupigwa risasi mjini Bujumbura
saa chache tu baada ya kuingia mwaka mpya.
Police wanasema amepigwa risasi alipokuwa akielekea nyumbani kwake eneo la Rohero .
Rais
wa Burundi Pierre Nkurunziza, ameapa kuchukua hatua kali za kisheria
kwa atakayepatikana na hatia ya kuhusika katika mauaji hayo.
Rais wa Burundi PIerre Nkurunziza amesema kuwa waliohusika watachukuliwa sheria kali.
Mamia ya watu , wakiwemo maafisa wa ngazi za juu katika jeshi
wameuawa tangu rais PIerre Nkurunziza kuwania urais kwa muhula wa tatu
2015, hatua ambayo wapinzani wanasema ni kinyume na sheria.
Lakini hii ni mara ya kwanza kwa waziri wa serikali kuuawa.
Kwa miezi kadhaa taifa hilo limekuwa tulivu.
COMMENT AND SHARE...................!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!