
Staa wa bongo movie ambaye maisha yake halisi yamekuwa yaki 'make
headlines' kwa kiasi kikubwa, Wastara, ametaja mambo matano ambayo
yamemuumiza zaidi maishani, na hatayasahau katika kipindi chote cha
maisha yake
Wastara akiwa kwenye kipindi cha Friday
Night Live cha EATV, amesema jambo la kwanza kubwa ambalo hataweza
kulisahau ni kuondokewa na wazazi wake wote wawili, jambo ambalo
lilimuumiza sana, na kuchangia kuvuruga akili na maisha yake japo Mungu
alimtia nguvu ya kuendelea kupambana katika maisha.
Jambo la pili asiloweza kusahau ni ajali
aliyoipata ambayo kwa kiasi fulani ilimsababishia ulemavu na kuwa
changamoto kubwa kukabiliana maisha, na la tatu ni kuondokewa na mume
wake aliyempenda sana, ambaye alikuwa ni muigizaji mwenzake, Sadiki Juma
maarufu kwa jina la Sajuki aliyefariki dunia mwezi Januari mwaka 2013.
Jambo la nne ni maamuzi aliyowahi
kuyafanya ya kutumia vyombo vya habari kuchagisha pesa kwa ajili ya
kumtibu marehemu mume wake Sajuki, kwamba jambo hilo alilazimika
kulifanya kutokana na shida lakini haikuwa ridhaa ya moyo wake, hivyo
lilimuathiri kwa kiasi kikubwa sana kisaikolojia, na hawezi kulisahau.
"Kukaa kwenye TV na kwenye Radio kwa
ajili ya kuchangisha pesa za kumtibia mume wangu kiliniumiza,
kiliniathiri sana akili yangu" Alisema Wastara.
Wastara ambaye alikuwa akitambulisha
rasmi movie yake mpya, alisema jambo la tano ambalo linagonga kichwa
chake mara kwa mara ni kitendo cha mashabiki wake kumchukulia tofauti na
alivyo kiuhalisia.
COMMENT AND SHARE........................!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!