Wanafunzi Wengine Elfu mbili(2000) Kupata Mikopo..:;
on
Get link
Facebook
X
Pinterest
Email
Other Apps
Zaidi ya wanafunzi 2,000 wenye sifa waliokosa mkopo watapewa mkopo mara
baada ya bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu kupitia rufaa za
wanafunzi hao na kuangalia endapo wameyafanyia marekebisho makosa
yaliyopelekea kunyimwa mkopo hapo awali.
Mwishoni mwa mwaka jana wanafunzi
walikosa sifa ya kupewa mikopo ya elimu ya juu, waligubikwa na majonzi
na vilio huku wengine wakipiga kambi katika ofisi za Bodi ya Mikopo ya
Wanafunzi wa Elimu ya Juu jijini Dar es salaam, kuomba kupatiwa mikopo
wakihofiwa kushindwa kuendelea na masomo yao licha ya kuwa wamechaguliwa
kuendelea na masomo ya elimu ya juu katika vyuo mbalimbali.
Veneranda Malima ambaye ni Afisa
Uhusiano wa bodi hiyo amesema baada ya kupitia rufani jumla ya wanafunzi
2,000 watapewa mikopo ambapo amewaondoa hofu wanafunzi waliokosa mikopo
na kuwataka kuambatanisha nyaraka na viambatanisho vyote muhimu kama
inavyotakiwa kwani lengo la bodi hiyo ni kuona wanafunzi wote wenye sifa
wanapewa mikopo na kuendelea na masomo yao.
COMMENT AND SHARE...............!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!