Walimu 765 wa elimu ya awali kutoka shule zote za Halmashauri za mkoa
wa RUVUMA wanapatiwa mafunzo kamilishi baada ya Taasisi ya Elimu
Tanzania kuboresha mtaala wa elimu ya mafunzo ya awali.
Mratibu wa Mafunzo hayo kutoka Taasisi hiyo, FREDRICK MKEBESI amesema
mafunzo hayo yanatolewa ili kuwajengea uwezo walimu wa elimu ya awali
yatakayowawezesha wanafunzi kujua kusoma, kuandika na kuhesabu.
Afisa Elimu wa mkoa wa RUVUMA, GHARAMA KINDERU amesema ni muhimu
walimu wakafuatilia vYema mafunzo hayo ili waweze kuwaelimisha walimu
wenzao waTAkaporudi shuleni.
Akifungua mafunzo hayo Katibu Tawala wa mkoa wa RUVUMA, HASSAN
BENDEYEKO amesema mafunzo hayo yanatolewa nchi nzima ili kuwezesha
watoto wote wa elimu ya awali kupata elimu stahiki.
COMMENT AND SHARE.......................!!!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!