Hii ni
mojawapo ya njia maarufu sana za kuzuia mimba na uzazi wa mpango sehemu
mbalimbali duniani na imekuwa ikitumika kwa muda mrefu na ufanisi mzuri. Pia, njia hii hujulikana kama vidonge vya majira au vidonge vya uzazi wa mpango na oral contraceptive pills kwa kiingereza. Vidonge hivi hufanya kazi kwa kutumia homoni za kutengenezwa za aina ya progestin na oestrogen. Homoni hizi hufanana na zile zinazotengenezwa mwilini.
Kuna aina mbili za vidonge vya kuzuia mimba;
- Vidonge vyenye progestin peke yake (Progestin Only Contraceptive Pills).
- Vidonge vyenye progestin na oestrogen (Combined Oral Contraceptive Pills).
Vidonge vyenye progestin na oestrogen (Combined Oral Contraceptive Pills) ndivyo vinanyopatikana kwa wingi na kutumika zaidi. Pia vina ufanisi zaidi.
Namna zinavyofanya kazi
Vidonge vyenye progestin na estrogen.
Vidonge hivi
humezwa kila siku kwa muda wa siku 28 kukamilisha mzunguko mmoja wa
hedhi. Vidonge vya siku 21 za mwanzo huwa na homoni za progestin na oestrogen kwa viwango tofauti na vya siku 7 za mwisho huwa na madini ya chuma.
Unywaji wa vidonge hivi katika siku 21 za mwanzo wa mzunguko huongeza homoni za progesterone na oestrogen kwenye damu, na hivyo kuzuia mimba kwa:
- Kuzuia mayai ya kike kuzalishwa na ovari
- Kuufanya ute wa kwenye shingo ya uzazi kuwa mzito na hivyo mbegu kushindwa kupita.
- Kuufanya ukuta wa mji wa mimba kutokuwa tayari kupandikiza kiinitete.
Baada ya 21 kupita, homoni za progestin na eostrogen hupungua kwenye mwili na hivyo ukuta wa mji wa mimba (endometrium) kuanza kubomoka ambako husababisha hedhi kutokea.
Vidonge vyenye progestin peke yake.
Huwa na vidonge 28 ambavyo humezwa kila siku. Vidonge hivi vyote huwa na homoni ya progestin peke
yake kwa viwango tofauti. Vidonge vya siku 7 za mwisho huwa na kiasi
kidogo cha homoni na hivyo ukuta wa mji wa uzazi hubomoka na mwanamke
kupata hedhi yake.
Huweza
kuzuia mimba kwa njia ambayo vidonge vyenye progestin na oestrogen
hufanya. Faida ya vidonge hivi huweza kutumika kwa wanawake wanaonyesha,
wenye shinikizo la damu la kupanda juu na wanaovuta sigara.
Namna ya kutumia
Vidonge hivi
huwa 28 kwa kila mzunguko wa hedhi, na kidonge kimoja humezwa kila
siku. Mtumiaji huchagua muda ambao utamfaa kuweza kunywa kidonge kila
siku katika muda huo bila kukosa.
Ni muhimu
kuzingatia muda wa kunywa dawa kila siku bila kukosa. Kutokunywa dawa
hata siku moja hupunguza ufanisi wa dawa kuzuia mimba!
Inashauriwa
kuanza kutumia vidonge hivi pale siku za hedhi zinapoanza ili kuondoa
uwezekano wa kutumia vidonge wakati kuna ujauzito na pia kuongeza
ufanisi wa dawa kufanya kazi.
Ni vizuri
ukaongeza na njia njingine ya uzazi katika mwezi wa kwanza wa kutumia
vidonge, kwa vidonge vinakuwa havijafikia ufanisi wake vizuri.
Hatua za kufanya unapokosa kunywa vidonge.
Ikitokea umekosa kunywa kidonge kimoja, kunywa mara unapokumbuka na kisha endelea na vidonge vingine kama kawaida.
Kama
haujakunywa vidonge 2, anza kunywa mara moja cha kwanza halafu cha pili
baada ya masaa 12 kisha endelea na vingine kama kawaida. Ongeza njia
nyingine ya kuzuia mimba kama kondomu kwa siku 7 zinazofuata kama
utafanya ngono kwani kuna uwezekano wa mimba kutokea kutokana na
kutokunywa dawa kwa mpangilio.
Kama umekosa
kunywa zaidi ya vidonge viwili, anza tena kutumia vidonge upya. Ni
muhimu pia ukaongeza njia ya ziada ya kukukinga na mimba au vidonge vya
dharura vya kuzuia mimba kama ulifanya ngono.
Tegemea
Kutokana na mabadiliko ya homoni yanayotokea hasa pale unapoanza kutumia vidonge hivi, mabadiliko yafuatayo yanaweza kutokea;
- kupata hedhi kidogo katikati ya mzunguko wako wa hedhi
- maumivu ya kichwa. Yakiwa makali sana onana na daktari wako.
Ufanisi
Njia hii ya
vidonge ina ufanisi mkubwa hana pale inapotumiwa kwa kufuata maelekezo
vizuri. Vidonge vinaweza kuzuia mimba kwa asilimia 99, kwa hiyo
unapotumia njia hii kwa makini uwezekano wa kupata ujauzito ni mdogo
sana!
Wanawake wasio shauriwa kutumia vidonge
Wanawake wenye historia ya magonjwa yafuatayo hawashauriwi kutumia dawa za kuzuia mimba za homoni;
- Ugonjwa wa moyo
- Shinikizo la damu la kupanda juu
- Matatizo ya damu kuganda kwenye mishipa (thromboembolism)
- Kiharusi
- Ugonjwa wa ini
Faida za vidonge
Pamoja na kuzuia mimba, vidonge hivi huwa na faida nyingine pia kwa mtumiaji. Faida hizi hujumuisha;
- Urahisi wa kutumia na haviathiri uwezo wa kufanya ngono
- Hupunguza maumivu na kiasi cha damu kinachotoka wakati wa hedhi.
- Ni rahisi kuacha pale mtu anapoamua, na uwezo wa kupata mimba kurudi.
- Hupunguza uwezekano wa kupata saratani ya kizazi, ovari na utumbo.
- Hutuliza mzunguko wa hedhi, ukae katika mpangilio mzuri.
Faida hizi huziwezesha vidonge kutumika kama matibabu kwa wanawake wenye matatizo yanayohusiana na hedhi.
Madhara ya vidonge
Matumizi ya
vidonge huweza kuleta madhara kwa mtumiaji, ingawa madhara mengi
yalihusishwa na vidonge vilivyokuwa na kiasi kikubwa cha homoni za oestrogen na progestin tofauti na sasa ambapo viwango vya homoni hizi vimepunguzwa.
- Hazikingi magonjwa ya zinaa.
- Hupunguza ubora wa maziwa mtoto anayonyonya kama mwanamke anayenyonyesha hii ni kwa vidonge vyenye progestinna oestrogen.
- Matiti kujaa na kuuma.
- Kukosa hedhi.
- Kunenepa na kuongezeka uzito
Onana na
daktari wako unapopata maumivu makali ya tumbo, kichwa, kifua au miguu
baada ya kuanza au kutumia vidonge vya kuzuia mimba kwa muda mrefu.
Muhimu!
Kabla ya kuanza kutumia njia hii onana na daktari kwa ajili ya
tathimini ya kiafya ili kujua kama una hatari ya magonjwa yasiyoruhusu
matumizi ya vidonge vya kuzuia mimba. Tumia vidonge vyenye homoni kidogo
(low-dosage pills), acha kuvuta sigara na zingatia mpangilio na ratiba ya kunywa vidonge kila siku!
By: Doctor Boaz (0767074124)
COMMENT AND SHARE.........................!!!!!!!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!