
Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya kidato cha
nne mwaka 2016 ambapo ufaulu umeongezeka kwa 2.56% kutoka 67.53% mwaka
2015 hadi 70.09% mwaka 2016.
Katibu Mtendaji wa barza hilo, Dkt
Charles Msonde amesema kati ya wanafunzi 408,372 waliofanya mtihani,
jumla ya wanafunzi 277,283 wamefaulu, wakiwemo wasichana 135,859 sawa na
asilimia 67.06 na wavulana 141,424 sawa na asilimia 73.26.
Kwa upande wa watahiniwa wa shule, Dkt
Msonde amesema kuwa watahiniwa 244,762 sawa na asilimia 70.35 ya
waliofanya mtihani wamefaulu ikilinganishwa na wanafunzi 240,996 sawa na
asilimia 67.91 waliofaulu mwaka 2015.
Aidha amesema baraza hilo limefuta
matokeo ya watahiniwa 126 waliobainika kufanya udanganyifu ikiwa ni
pamoja na watahiniwa 58 wa shule, 58 wa kujitegemea na watahiniwa 10 wa
QT. Pia baraza hilo limefuta matokeo ya mtahiniwa mmoja aliyebainika
kuandika matusi kwenye karatasi yake ya majibu.
Kwa upande wa ubora wa ufaulu, amesema
watahiniwa wa shule wenye ufaulu mzuri wa Daraja la kwanza hadi la tatu
ni 96,018 sawa na asilimia 27.60
Kwa upande wa masomo, amesema ufaulu
katika masomo ya History, Geography, Kiswahili, English Language, Basic
Mathematics, Physics, Biology, Commerce na Book keeping umepanda kwa
kati ya asilimia 0.12 na 8.08 ikilinganishwa na mwaka 2015.
Somo lililoongoza kwa ufaulu ni
Kiswahili ambapo asilimia 77.75 wamefaulu na somo la mwisho ni Basic
Maths ambalo asilimia 18.12 ya watahiniwa wa shule wamefaulu.
Kati ya wanafunzi 10 bora kitaifa,
wanafunzi 5 ni wasichana na 5 ni wavulana wakiongozwa na Alfred Shauri
kutoka Feza Boys ya Dar es Salaam
Kati ya shule 10 zilizofanya vibaya
kitaifa, shule 6 zinatoka katika mkoa wa Dar es Salaam wakati shule
iliyoongoza ikiwa ni Feza Boys ya Dar es Salaam. Pia katika shule kumi
bora kitaifa, hakuna shule ya serikali
Mkoa wa Njombe umeongoza katika mikoa 10
iliyofanya vizuri zaidi kitaifa ukifuatiwa na Iringa, Kagera, Kigoma na
Kilimanjaro huku halmashauri za Bukoba Mjini, Njombe, Kakonko, Kahama
na Wang'ing'ombe pia zikiibuka vinara
COMMENT AND SHARE...................!!!!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!