Rais mteule wa Marekani Donald Trump amemteua mkwe wake Jared Kushner, kuwa mshauri mwandamizi wa Ikulu ya nchi hiyo.
Kushner
mwenye umri wa miaka 35 ambaye amemuoa binti mkubwa wa Trump, Ivanka,
alifanya kazi kubwa wakati wa kampeni za uchaguzi, zilizomuwezesha Trump
kushinda.
Majukumu ya kazi yake yanatarajiwa kuhusika na masuala
ya sera za nje na ndani ya nchi, ikiwemo masuala ya biashara na
Mashariki ya Kati.
Uteuzi huo hauhitaji kuthibitishwa na bunge la seneti.
Lakini hata hivyo baadhi ya wachambuzi wanahoji kama uteuzi huo utakiuka sheria ya kupinga upendeleo wa undugu katika ajira.
Jared
Kushner hata chukua mshahara kwa uteuzi huo wa Ikulu ya Marekani na
itampa nafasi ya kumfanya kuwa huru na maslahi ya shughuli zake za
kibiashara.
COMMENT AND SHARE.................!!!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!