Klabu ya Tottenham Hotspur ya
Uingereza imetoa picha za kwanza za uwanja wa klabu hiyo ambao
unaendelea kujengwa kaskazini mwa London.
Uwanja huo, ambao
utatoshea mashabiki 61,000, utakuwa ndio mkubwa zaidi wa soka katika
jiji kuu la London utakapofunguliwa mwaka 2018.
Miongoni mwa
mengine, utakuwa na baa kubwa zaidi ya kuhudumia watu wote uwanjani
Uingereza. Aidha, viti vyake vitakuwa na mitambo ya kubadili viwango vya
joto.
Kutakuwa pia na kiwanda kidogo cha kutengeneza pombe na pia kiwanda kidogo cha kuoka mikate na keki.
Mwenyekiti wa Spurs amesema uwanja huo utaleta "taswira mpya kwa michezo na burudani".
Uwanja huo utakuwa na sakafu iliyopandwa nyasi ambayo inaweza kuondolewa na chini yake kutokee sakafu ya mkeka.
Hilo litawezesha uwanja huo kuwa mwenyeji wa mechi za kandanda, NFL, matamasha pamoja na hafla nyingine.
Miongoni mwa mengine, uwanja huo utakuwa na:
- Njia iliyozingirwa kwa kioo cha
kutumiwa na wachezaji kuingia uwanjani. Hii itawawezesha mashabiki
kutazama yanayojiri kabla ya mechi.
- Eneo la kuuzia bia la umbali wa 285ft (86.8m) ambapo kila mtu atauziwa
- Mfumo mpya wa kusambaza bia ambao utawawezesha wauzaji kutoa painti 10,000 za bia kila dakika.
- Viti vitakuwa na mitambo ya kuongeza joto na sehemu za kuwezesha mtu kutumia vifaa vya USB.
- Kutakuwa na sehemu moja ya kuketi watu 17,000, ambayo itakuwa kubwa zaidi Uingereza.
Ujenzi wa uwanja huo utagharimu £750m lakini utabuni nafasi
3,500 za ajira eneo hilo utakapokamilishwa, kwa mujibu wa klabu hiyo.
Watu wataweza kuwatazama wachezaji wakiingia na kutoka uwanjani kupitia kioo
Watu kwenye mgahawa wa orofa ya tisa wa Sky Lounge wataweza kutazama vizuri yanayojiri
Timu hiyo ambayo kwa sasa mkufunzi wake ni Mauricio Pochettino
itahitajika kutumia uwanja mwingine msimu wa 2017-18 uwanja huo
unapojengwa.
Chama cha Soka Uingereza(FA) kimewapa Spurs fursa ya
kukodi uwanja wa Wembley ingawa pendekezo hilo limepingwa na mbunge wa
chama cha Conservative Bob Blackman.
Chelsea, ambao wanajenga
uwanja mpya wa Stamford Bridge kuweza kutoshea mashabiki 60,000 pia
wamependekezewa uwanja huo wa Wembley.
Klabu za Uingereza zimekuwa zikijizatiti kuimarisha uwezo wa viwanja.
Miaka kumi iliyopita Arsenal walijenga uwanja wao wa Emirates unaotoshea mashabiki 60,000.
West Ham walihamia uwanja wao wa Olimpiki unaotoshea mashabiki 57,000 eneo la Stratford, London mashariki.
Uwanja
wa sasa wa Stamford Bridge unaotoshea mashabiki 41,663 ndio wa saba kwa
ukubwa miongoni mwa viwanja vinavyotumiwa na klabu za Ligi ya Premia.
Uwanja wa Old Trafford unaotumiwa na Manchester United hutoshea mashabiki 76,000.
COMMENT AND SHARE...............!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!