Idadi ya waliofariki kutokana na
ajali ya Treni kusini mashariki mwa India imefikia zaidi ya watu watu
30. Watu wengine zaidi ya 50 wamejeruhiwa baada ya Treni hiyo kuacha
reli na
kubingiria ilipokuwa safarini kati ya Jagdalpur na
Bhubaneswar katika jimbo la Andra Pradesh usiku wa Jumamosi.Maafisa wa
uokozi wamesema watu wengi wangali wamekwama ndani
ya mabehewa ya Treni hiyo na wanahofia idadi ya waliofariki huenda ikaongezeka. Kilichosababisha ajali hiyo bado haijabainika.
Ajali ya Treni hutokea mara kwa mara nchini India kutokana na miundo mbinu duni na kuchakaa kwa reli.
Mwezi Novemba mwaka jana zaidi ya watu 140 walifariki kutokana na ajali nsawa na hii kaskazini mwa jimbo la Uttar Pradesh
Msemaji
wa kitaifa wa uchukuzi wa reli Anil Saxena amesema maafisa wa uokozi
wanaendeleza juhudi za kuwafikia manusura wa ajali hiyo.
COMMENT AND SHARE...............!!!!!!1
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!