Spika wa Bunge JOB NDUGAI ameishauri serikali, mashirika na idara mbalimbali kuharakisha utaratibu wa kuhamia mkoani DODOMA.
Akizungumza katika mahojiano maalum na TBC mjini DODOMA, NDUGAI
amesema kwa kufanya hivyo watakuwa wametekeleza azma ya serikali ya
kuhamia makao makuu pamoja na kuongeza kasi ya ukuaji mkoa huo na taifa
kwa ujumla.
Aidha NDUGAI mkutano wa Sita wa Bunge la KUMI na MOJA wa bunge
unaanza kesho pamoja na mambo mengine wabunge wateule Profesa
PALAMAGAMBA KABUDI na ABDALLAH BULEMBO MAJURA wataapishwa.
Spika pia amezungumzia shughuli mbalimbali zitakazofanyika wakati wa vikao hivyo vya bunge,
Waziri mkuu KASSIM MAJALIWA tayari ameshawasili mkoani DODOMA kwa ajili ya kuhudhuria vikao hivyo vya bunge.
COMMENT AND SHARE..........................!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!