Msanii wa muziki wa bongo fleva Vanessa Mdee amefunguka na kuweka wazi
kuwa mara nyingi huwa wanagombana na mpenzi wake huyo Jux kutokana na
tabia yake ya kuchelewa kujibu jumbe fupi au hata kupokea simu zake.
Vanessa
Mdee alisema haya kwenye kipindi cha 'Ngaz kwa Ngaz' kinachorushwa na
ting'a namba moja kwa vijana EATV na kudai kuwa Jux kwenye suala la simu
amekuwa mvivu sana na ndiyo jambo linaloleta tofauti kati yao.
"Mvivu wa simu amefarakanishwa na simu
yake huyu jamaa, hata kwenye kujibu txt au kupokea simu hana ushirikiano
na simu kabisaa kwa hiyo tunagombanaga mara nyingi kuhusiana na
communication" alisema Vanessa Mdee .
COMMENT AND SHARE.............................!!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!