Welcome to VIVAX MEDIA, feel free to Comment and dont forget to Share (also please Click on the YOUTUBE, YOUTUBE, YOUTUBE button above/bellow the page).....!! Welcome to VIVAX MEDIA, feel free to Comment and dont forget to Share (also please Click on the YOUTUBE, YOUTUBE, YOUTUBE button above/bellow the page).....!! Welcome to VIVAX MEDIA, feel free to Comment., dont forget to Share (also please Click on the YOUTUBE, YOUTUBE, YOUTUBE button above/bellow the page).....!! Welcome to VIVAX MEDIA, feel free to Comment., dont forget to Share (also please Click on the YOUTUBE, YOUTUBE, YOUTUBE button above/bellow the page).....!!

Simba Yamnyooshea Yanga Njia ya Kuchukua Ubingwa..:;

Tokeo la picha la simba vs azam 2017           Vinara wa ligi kuu Tanzania bara hivi sasa ni kama inamnyooshea mtani wake Yanga njia ya ubingwa baada ya leo kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa matajiri wa Jiji la Dar es Salaam, Azam FC, katika dimba la Taifa Dar es Salaam.                  
Yanga inaweza kukalia kiti cha uongozi endapo itashinda mechi yake ya kesho ambapo itafikisha pointi 46, ikiwa ni point 1 mbele ya Simba na hivyo kunogesha zaidi mbio za ubingwa huku Yanga ikiwa kileleni.
Katika mchezo wa leo, alikuwa ni mshambuliaji matata anayefahamika kwa sifa kuu ya urefu, nguvu na jicho la kuliona goli vizuri, John Bocco kutoka Azam FC ndiye aliyeibeba timu yake na kuibuka na ushindi huo kwa bao pekee alilopachika kwa shuti kali katika dakika ya 70.
Bocco amefunga bao hilo baada ya kumzidi uwezo beki wa kutumainiwa wa Simba, Method Mwanjali baada ya kupigwa 'kaunta' moja ya hatari na Mwanjali kushindwa 'kukontrol' mpira ambapo Bocco alikuwa karibu na kufanikiwa kuunasa na kumtoka Mwanjali, na kuachia shuti upande wa kulia wa Agyei lililojaa wavuni.
Bao hilo lilifungwa ikiwa ni baada ya Simba kufanya mabadiliko kwa kuwatoa Jamal Mnyate, Javier Bukungu na Juma Luizio na nafasi zao kuchukuliwa na Kichuya, Ajibu na Mavugo huku upande wa beki Simba ikibaki na mabeki watatu kutokana na nafasi ya Bukungu kuwa wazi licha ya kujaribu kuzibwa na Mzimiru, upande ambao ndiko bao lilikopitia.                        
John Bocco
Licha ya Simba kuzidisha mashambulizi, lakini umahiri wa mlinda mlango wa Azam Aishi Manula ulizima kabisa ndoto za Simba kuambulia japo point moja kwa kuokoa michomo kadhaa iliyokuwa dhahiri ikiingia wavuni
Huu unakuwa ni mwendelezo wa Bocco kuzitesa Simba na Yanga na mpaka sasa anakuwa ndiye mchezaji ambaye ameifunga Simba mabao mengi zaidi ambapo mpaka sasa ameifunga mabao 19 katika historia ya Simba.
Hiki ni kipigo cha pili mfululizo Simba inapata kutoka kwa Azam baada ya kile cha bao 1-0 katika fainali ya Kombe la Mapinduzi
Kwa matokeo haya Simba bado ipo kileleni mwa ligi ikiwa na pointi 45, ikifuatiwa na Yanga mwenye pointi 43 ambayo kesho itashuka dimbani kuvaana na Mwadui FC, na Azam imefikisha pointi 36 ikiwa nafasi ya 4.        




COMMENT AND SHARE...................!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!

Comments

Facebook Twitter Youtube