Shule ya watu waliobadili jinsia yafunguliwa India:;
on
Get link
Facebook
X
Pinterest
Email
Other Apps
Shule ya watu waliobadili jinsia
imefunguliwa katika mji wa Kochi nchini India , ili kuwasaidia watu
wazima walioacha shule kukamilisha masomo.
Watu waliobadili jinsia hushambuliwa nchini India na nusu yao hukosa kukamilisha masomo.
Shule ya kimataifa ya Sahaj ndio shule ya kipekee nchini India.
Itawakaribisha wanafunzi 10 walio na kati ya umri wa miaka 25 hadi 50.
Wanafunzi
hao wataandaliwa kufanya mitihani ya 10 na 12 katika bodi ya mitihani
ambayo hufanywa wakati mwanafunzi anapofikisha umri wa kati ya miaka
15-16 ama 17- 18 mtawalia.
Mtaala pia utashirikisha mafunzo ya kiufundi.
Mwanaharakti
wa watu wanaobadili jinsia Vijayraja Mallika ambaye anasimamia shule
hiyo ameambia BBC: Shule hii inalenga kuwasaidia watu waliobadili
jinsia kupata kazi nzuri na kuishi katika maisha ya heshima.
''Tumesajili
wanafunzi sita kufikia sasa wote wakiwa wanaume waliobadili kuwa
wanawake kutoka kwa maombi 14.Kati ya viti kumi vilivyopo ,tumehifadhi
kiti kimoja kwa mwanamke anayebadili jinsia kuwa mwanamume pamoja na
kimoja cha mlemavu''.
COMMENT AND SHARE.......................!!!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!