
Rapa Roma Mkatoliki leo kwenye kipindi cha Planet Bongo amefunguka na
kutaja orodha ya wasanii wake wa tano wa hip hop Bongo ambao
anawasikiliza na kuwakubali zaidi kutokana na kazi zao.
Roma
Mkatoliki kwa kuanza alimtaja Rapa Roho Saba na kusema anamsikiliza
sana na kumkubali sana na watu watashangaa kwanini amemtaja Roho Saba
ili hali ana ngoma mbili tu ila yeye anasema anazisikiliza sana hizo
kazi mbili kuliko kazi nyingine nyingi kutoka kwa wasanii wengine.
"Kiukweli nawasikiliza sana wasanii
wengi wa Hip hop Bongo lakini kwa kuwa nimepewa nafasi ya kutaja wasanii
watano tu wa kwanza nitaanza na mwanangu Jaco Roho Saba, mchizi ana
ngoma mbili tu lakini nazisikiliza sana, namkubali sana Jose Mtambo,
Prof Jay pia maana kitambo namsikiliza na alini'inspire' toka enzi hizo
mpaka leo. Wengine ni Saigoni pamoja na Hashim Dogo" alisema Roma
Mkatoliki.
COMMENT AND SHARE...............!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!