
Anaejua kuna njaa nchi hii ni Rais, mimi ndio ninayejua wapi kuna njaa
na wapi hakuna. Tanzania hii haina njaa wala watu hawana njaa,anasema
Rais JPM kutoka Simiyu
Wanaotangaza kuna njaa ni watu wanaolipwa pesa na wafanyabiashara na
wanasiasa ili kusema nchi ina njaa na ukame wa kuuwa watu na mifugo.
Yapo magazeti yanayotumiwa na wafanyabiashara na wanasiasa ili kusema
Tanzania kuna njaa. Kuna mfanyabiashara mmoja ana tani 25,000 za mahindi
bandarini anataka aingize bila kodi kwa kisingizio cha njaa Tanzania.
Rais anasema ameagiza alipe kodi na asipitishe mahindi hayo bure kwa
kisingizio cha njaa, Tanzania haina njaa.
Kuna mfugaji mwingine walimlipa hela wanasiasa huko Mvomelo, akaenda mbele ya Tv na kusema ana mifugo inakufa kwa ukame.
"Nimeagiza wamwambie auze hizo ng'ombe ili aepukane na ukame. Huwezi
kuwa na ng'ombe karibu elfu na zaidi na wanakufa ng'ombe 16 unaanza
kulialia badala ya kuuza upate hela ya kula na ujikimu kimaisha."
Rais anasema hatapeleka chakula Simiyu na Bariadi eti kisa ukame.
Wananchi walitakiwa kujua kama mvua ni ndogo basi walime mazao
yanayostahimili ukame na si kulazimisha kulima mahindi yanayohitaji mvua
nyingi. JPM anasema msema ukweli ni mpenzi wa Mungu na yeye anasema
ukweli kuwa hataleta chakula popote kwa sababu ni wanasiasa na
wafanyabiashara ndio wananunua magazeti kutangaza njaa.
Rais kamuumbua Dr Kamani, mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu anayemtaka
Rais aruhusu kuingiza mifugo kwenye hifadhi, wakati yeye akiwa waziri wa
Mifugo wakati wa JK hakufanya hivyo, sasa kama sio unafiki ni nini? JPM
anasema yeye sio mnafiki, hataruhusu mifugo kuingia kwenye hifadhi kwa
sbb ya sifa za kisiasa huku akiharibu mazingira.
Rais anasema Watanzania walizoea kuambiwa maneno "matamu matamu" na
wanasiasa huku muda ukienda bila kuwa na maendeleo. Yeye anataka
watanzania wasahau maneno matamumatamu. Ataongea ukweli tu,tena ukweli
mchungu hata kama utawaudhi watu, kama ni jiwe atasema jiwe na sio
mchanga mgumu uliokusanyika pamoja.
Rais amewaomba Watanzania wazidi kumuombea, wapo "wapinzani" wake
wanamsimanga kwa kununua ndege, na wakati kwa miaka mingi Tanzania
haikuwa na ndege, na hao wanaomkosoa ndio hao hao wanaokimbilia
kuzipanda.
Baadae Rais akamuita mhandisi Maji wa Mkoa wa Simiyu ili aje aelezee
mpango wa Maji kutoka Ziwa Victoria kuja mkoa wa Simiyu na Wilaya
zake... Mhandisi hakutoa majibu mazuri, akaja RAS ambaye akasema kikwazo
ni mlima wa Ngasamo ambao una madini ya Nikel(?) ambao ndio ilipaswa
kuwa na tank la kuleta maji. Eneo hilo tayari kuna muwekezaji na
hawawezi kuweka tank.
Rais ameamuru mgodi huo usipewe leseni na huyo muwekezaji apewe taarifa
kuwa huo mgodi haupo tena na watu wapewe eneo la kuweka Tank. Amemuagiza
Kamishna wa madini aifute leseni na ujumbe umfikie Waziri wa Madini na
autekeleze.
Na mwisho Rais amesisitiza watu wafanye kazi,hakuna wa kugawiwa chakula
bure.Hawezi akawasomeshea watoto bure,ajenge barabara, anunue ndege,
ajenge hospitali na kuweka madawa ktk hospital, alete huduma ya maji na
bado watu wakae tu na kusubiri eti serikali itawatafutia chakula.Watu
wafanye kazi ili wapate chakula na si kusubiri chakula cha serikali.
"SERIKALI YANGU HAITATOA CHAKULA, NINAPOSEMA SILETI CHAKULA SILETI
KWELI, WALA SIMUNG'UNYI MANENO NA SITALETA KWELI, MLIZOEA MANENO MATAMU
SASA MIMI SINA MANENO MATAMU" alisisitiza Rais Magufuli.
Mwishoni Rais amemalizia kwa kusema: "
Naweza kuwa sio mwanasiasa mzuri sana, Lakini ipo siku mtakuja kunikumbuka"
COMMENT AND SHARE....................!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!